HOME
MWANANCHI
Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu mkazi wa Buza,Dar es salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya.
Damu na mkojo vya mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa vilichukuliwa na kupimwa katika Maabara ya hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili majibu yalitoka yakionyesha kuwa alikua na chembechembe za dawaza kulevya aina ya Heroine.
Taarifa za kitabibu ziaonyesha Heroini katika mwili wa binadamu huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne endapo dawa hizo zilitumika na muhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano.
Mtaalamu wa tibawa hospitali hiyo Elifasi Mritu anasema ‘Ni kweli ukitumia dawa hizo wakati wa kunyoshesha ama ukiwa na mimba mtoto naye huathirika’.
Mama wa mtoto huyo Zena au maarufu kama Zerish alisema alipata ujauzito wakati akitumia dawa hizo za kulevya hadi sasa na anapovuta ama kujichoma mtoto wake pia hupata ‘stimu’kwa sababu hupata dawa hizo kupitia maziwa anayonyonya na hivyo wote wawili kulala fofofo sehemu yoyote.
MWANANCHI
Maalim Hassan Hussein ambaye nimtoto wa aliyekua mtabiri maarufu nchini Sheikh Yahya Hussein ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani,likiwemo la kufariki gafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenyembio za kuwania urais mwakani.
Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka gafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.
Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini pia atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake.
Kuhusu uchaguzi Mtabiri huyo alisema kundi la vijana na wazee nyota inaonyesha kwamba watakaofaidika ni vijana lakini kuna wazee pia watakaoweza kufaidika ambao ni wale wenye sura za babyface au wenye kupenda mambo ya ujana.
Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi yenye kuwa na amani na utulivu ni kuwa na rais kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.
MWANANCHI
Waliokua wafanyakazi wa Shirika la ndege ATCL wamefungua madai ya kuomba kukazia hukumu katika mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Kazi,wakiomba kukamata na kuliuza jengo la ATC House ili wafidie malimbikizo ya mishahara yao.
Kwa mujibu wa madai hayo namba 385 ya mwaka 2014 kupitia wakili wao Benjamini mwakagamba,pia waliomba mahakama hiyo kuteua dalali atakayeliuza jengo hilo lililopo eneola Posta.
Mmoja wa wafanyakazi hao kapteni Suel Mjungu alisema anadai sh.72,757,042.48 huku mwenzake Msami akidai sh.114,244,807.3 ambazoni za awamu ya kwanza walitakiwa kulipwa Oktoba 2013 lakini hadi sasa hawajalipwa.
NIPASHE
Mbio za urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM zimechukua sura mpya baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza rasmi kuwania kiti hicho mwakani.
Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapigakura wake Mkoani Singida alisema muda Tanzania kupata maono mapya umefika.
“Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika,nitachukua hatua ya kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika,maelfu ya watu watanisindikiza wanaume,wanawake,vijana kutoka Mikoa mbalimbali.
“Wale wote waliotangaza nia kupitia chama changu kazi zao lazima zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe itazipima”alisisitiza.
Alisema pindi Rais Kikwete atakapohitimisha utawala wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya.
HABARILEO
Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe amesema wiki ijayo atatanfaza majina ya wafanyakazi wa kampuni ya Reli Tanzania TRL watakaofukuzwa kazi kutokanana kutokua na tija kwenye kampuni.
Aidha alisema huduma ya usafiri wa Reli ya kati,zitaanza mwishoni mwa mwezi wa Januari hivyo kuwataka wananchi wanaoishi kandokando ya Reli kuondoka kwani wanahatarisha maisha yao.
“Serikali inawekeza ili tuone tija,na kama tija haionekani basi uongozi wa juu una shida,hatuwekezi pesa na kunyima sekta nyingine halafu reli ikabaki vile vile,fanyeni kazi kwa ubunifu la,nitafukuza wote”alisema Mwakyembe.
“Shirika limejaa mtandao wa wezi tuukiwemo wa mafuta,nimewaonya iliyopita,kazi yenu wizi tu na kulifanya Shirika likose tija,leo tunaleta vifaa vya mabilioni ya kodi za wananchi,kichwa kimoja cha treni kinagharimu bilioni 7,halafu kinapinduka kwa uzembe uzembe tu”alisema.
DIRA YA MTANZANIA
Ujenzi holela uliofanywa na wafanyabiashara wa soko la Mchikichini eneo la Karume jijini Dar es salaam unaweza kusababisha maafa zaidi endapo kutatokea tena maafa ya moto.
Soko hilo ambalo linategemewa na wakazi wengi wa Jiji la Dar es salaam kutokana na kuuza bidhaa nyingi za mitumba liliwahi kuungua mwezi Juni na kuteketeza mali za watu na kusababisha hasara kubwa.
Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo na miundombinu isiyokidhi mahitaji ya uokoaji ukiwa kutatokea ajali ya moto kutokana na ujenzi holela wa mabanda ya kuuza mitumba kwani hakuna nafasi ya kupita gari la kutoa msaada linapotokea tatizo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala waliahidi kwamba wangewajengea wafanyabiashara hao eneo la kisasa mara baada ya kutokea kwa ajali moto lakini kwa sasa Serikali haina uwezo wa kuwajengea upya na kufidia hasara zilizopatikana.
Hizi ni zile Story zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 29, 2014

Chapisha Maoni