HOME
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeagiza Sukari kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho Mei 11, 2016.
Ametoa kauli hiyo leo mchana Mei 10, 2016 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi wa sukati ambayo
imekwishawasili nchini Waziri Mkuu alisema tani 2000 zitapelekwa (Mikoa
ya kaskazini), tani 3,000 (Mikoa ya kanda ya ziwa), tani 2,000 (Mikoa ya
Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya
kanda ya kati).
‘Tani
nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke
bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia
Jumatatu.Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi
huu au mapema mwezi Juni’– Waziri Mkuu
Amesema anawataka watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache ‘Mheshimiwa
Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwa
Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwasababu viwanda vyetu vinatarajia
kuanza uzalishaji ifikapo Julai’- Waziri Mkuu
Waziri huyo amewataka wasambazaji wa
sukari waziuze kwa wafanyabiashara wadogo ili wao wawauzie wananchi kwa
bei elekezi ya Sh.1800, pia amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya
kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale
waliohodhi bidhaa hiyo.
‘Serikali
imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo,
Ngerengere na Kigoma huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya Sukari
na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi utakapoweza kuimaliza
hii gap iliyopo’- Waziri Mkuu
Chapisha Maoni