Majibu ya Ridhiwani Kikwete kuhusu NEC na kwa wanaosema anamiliki vituo vya mafuta.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu
vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’
‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’
‘Kuna kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??’
‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi kama watu wengine.
Chapisha Maoni