KIKONGWE
aliyejulikana kwa jina la Sayi Nyenje (75) mkazi wa kijiji cha Mwagata
kata ya mwamalilli manispaa ya shinyanga ameuwawa kwa kucharangwa
mapanga sehem mbali mbali za mwili wake.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba limetokea jana majira ya saa tano
usiku nyumbani kwa kikongwe huyo.
Kamanda Kamugisha amesema wakati kikongwe huyo akiwa amelala na wajukuu
zake wawili ghafla alivamiwa na watu wawili ambao hawakuwafahamu na
kumcharanga na mapanga shingoni na mabegani hali iliyopelekea kifo
chake.
Amesema jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia Joel Machia (45)
mkazi wa Mwamalili anashikiliwa kwa tuhuma hizo na kwamba uchunguzi
unaendelea.
Aidha kamanda Kamugisha amesema jeshi la polisi katika uchunguzi wa
awali limebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kugombea
mashamba.
Chapisha Maoni