HOME
JAMII YATAKIWA KUACHA KUFUMBIA MACHO VITENDO VIOVU DHIDI YA WATOTO
Aidha Mpesya amewataka wazazi kuepuke kupokea vitu vidogovidogo pamoja na kuwaoza watoto wao wakiwa katika umri mdogo huku wakiwa bado wanasoma ni kukiuka sheria ambapo ameahidi kuyatafuta majalada ya kesi hiyo na kuesma endapo iliendeshwa kinyume utaratibu itarudiwa.
Kwa upande wake Afisa
Mradi kutoka shirika la CARE INTERNATIONAL,Gega Bujeje amesema shirika
lake linajihusisha katika kutoa elimu ya Afya na uzazi pamoja kupinga
mimba na ndoa za utotoni na amedai kuwa wanakumbana na changamoto nyingi
katika jamii kutokana na uelewa mdogo wa wazazi.
JAMII YATAKIWA KUACHA KUFUMBIA MACHO VITENDO VIOVU DHIDI YA WATOTO
Jamii wilayani Kahama
mkoani Shinyanga imetakiwa kuwa na uelewa juu vitendo viovu
wanavyotendewa watoto wa kike na baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na
kutovifumbia macho ili kuisaidia Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo
na mkuu wa Wilaya hiyo,Benson Mpesya wakati akizungumza na wandishi wa
Habari ofisini kwake juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike
hasa kutokana na kukithili kwa mimba za utotoni huku wakiwa mashuleni.
Aidha Mpesya amewataka wazazi kuepuke kupokea vitu vidogovidogo pamoja na kuwaoza watoto wao wakiwa katika umri mdogo huku wakiwa bado wanasoma ni kukiuka sheria ambapo ameahidi kuyatafuta majalada ya kesi hiyo na kuesma endapo iliendeshwa kinyume utaratibu itarudiwa.
Hivyo
ameitaka jamii kwa kushirikiana na Serikali kufanya kazi na shirika
hilo ili kuibua maovu yanayoendelea kwenye jamii hiyo ili kuleta
mabadiliko katika usawa wa kijinsia.
Source:Kadama Malunde/Paulina Juma
Chapisha Maoni