Klabu ya Real Madrid ya Hispania usiku wa May 28 2016 ilicheza mchezo wake wa fainali ya Klabu Bingwa barani dhidi ya Atletico Madrid katika jiji la Milan Italia uwanja wa San Siro, hiyo ilikuwa fainali inayohusisha timu kutoka jiji moja la Madrid, hivyo upinzani ulikuwa mkubwa.
Katika mchezo huo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid walifanikiwa kutwaa Kombe lao 11, huku Atletico wakiambulia kushindwa kuweka rekodi ya kutwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao, Real Madrid walifanikiwa kuifunga Atletico kwa mikwaju ya penati 5-3, hiyo ni baada ya dakika 12o kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Baada ya Ubingwa Real Madrid waliwasili Hispania katika jiji la Madrid wakiwa na Kombe lao la 11 la UEFA.
Chapisha Maoni