Mashindano ya Olimpiki ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne yakihusisha michezo tofautitofauti na ikiwa imesalia miezi mitatu kufanyika kwa mashindano hayo huko mjini Rio de Jenairo Brazil msimu huu lakini taarifa zinazoripotiwa ni kuwa msimu huu huenda yakaingia dosari baada ya madaktari 150 Duniani pamoja na wataalamu wa maswala ya afya kuungana pamoja kupinga mashindano kufanyika.
Madaktari hao wametahadharisha juu ya usalama wa afya za wachezaji, waandishi wa habari pamoja na wote watakaohusika katika mashindano hayo. Wamependekeza mashindano hayo yaahirishwe kwa sasa mpaka kutakapokuwa na usalama wa kiafya nchini humo au yafanyike sehemu nyingine tofauti na Brazil. Sababu kuu ni kutokana na uwepo wa virusi vya zika nchini Brazil wakihofia kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo.
Virusi vya Zika uambukizwa kwa kung’atwa na mbu aina ya Aedes aegypti ambaye pia usambaza homa za dengue pamoja na homa ya manjano ambapo muathirika wa virusi vya zika hujifungua mtoto mwenye kichwa kidogo kupita kiasi hali hiyo ikiambatana na maumivu makali ya kichwa, ngozi kusinyaa, misuli kukaza pamoja na homa za mara kwa mara.
Chapisha Maoni