HOME
HATIMAYE Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kukata
mzizi wa fitina kwa kuunda Kamati Maalumu iliyopewa kazi ya kuchunguza
mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kupunguza ajali za barabarani.
Kuundwa kwa kamati hiyo ambayo ni muhimu katika kipindi hiki, kunafuatia malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali juu ya ajali zinazotokana na sababu mbalimbali, kubwa zikionekana ni kutokana na mwendo kasi, umakini mdogo wa madereva na uswaiba uliojengeka kati ya madereva, wamiliki hasa wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo na maskari wa Usalama Barabarani.
Akizungumza baada ya mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji jana, Dk Mwakyembe alisema kamati hiyo itafanya kazi usiku na mchana kwa wiki mbili na Oktoba 5 yeye, mawaziri wenzake, Gaudentia Kabaka wa Kazi na Ajira na Mathias Chikawe wa Mambo ya Ndani watakutana ili watoe maamuzi mbalimbali yatakayosaidia kupunguza tatizo hilo.
Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, kamati hiyo itaundwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi ambaye pia atakuwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna wa Mapato Nchini (TRA), Kamishna Mkuu wa Wakala wa Bima, na Mwakilishi wa Wamiliki wa Mabasi (Taboa).
Mwekyembe pia alisema kamati inawahusisha wasimamizi mbalimbali wa sekta ya usafirishaji akiwamo Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mtendaji Mkuu wa VETA, Mtendaji Kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa na Mwakilishi wa Wamiliki wa Malori (TATOA).
Tunaamini kamati hiyo imesheheni watu ambao wamebobea katika sekta ya usafirishaji na Watanzania wanategemea kupata suluhisho la kudumu la kukomesha ajali za barabarani ambazo kila kukicha zimekuwa chinja chinja kwa Watanzania wasiokuwa na hatia.
Tumeshuhudia katika kipindi cha muda mfupi, ajali nyingi zikifuatana huku Serikali ikihangaika kukomesha tatizo hilo bila mafanikio.
Kamati hii italeta mwanga hasa ikiangaliwa wale ambao wameteuliwa kwa kuwa wao ni wadau wakubwa wa usafiri. Jana gazeti hili lilikuwa na habari iliyokuwa ikishutumu Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuwa kimekuwa chanzo kikubwa cha ajali hizi.
Hoja hii iliibuliwa katika mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji juzi ambao ulikuwa ukizungumzia namna ya kumaliza ajali ambapo trafiki ndio walionyoshewa vidole zaidi.
Kazi hii ikikamilika, tunaamini wajumbe watagusia pia na suluhisho la nini kifanyike baada ya kumaliza kazi yake kwa kuwa watakuwa tayari wana majumuisho ya masuala mengi yanayogusa sekta hii nyeti ya usafiri na ndipo tunaposema tume hii imeundwa kwa wakati muafaka.
Hata hivyo, tungependa kusisitiza jambo la msingi kwamba, Tanzania mara nyingi imekuwa ikiunda tume nyingi baada ya matukio hasa yanayogusa jamii na matokeo yameishia kwenye makabrasha.
Tunaomba hii Kamati ifanye kazi ambayo itaondoa tatizo kwani Watanzania wameshachoshwa na ajali hizi ambazo nyingine zinaonekana wazi zinatokana na uzembe wa usimamizi katika sekta hii ya usafirishaji.
Kamati ya Mwakyembe ije na suluhisho la ajali Tanzania

Chapisha Maoni