HOME
Bomoabomoa ilianza mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam hasa ya mabondeni ikiwemo maeneo ya kando na mto msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya kesi inayopinga ubomoaji wa nyumba takribani 2619 za wakazi wa Tabata Segerea kufunguliwa.
Sasa April 22 2016 maamuzi ya kesi hiyo yalitolewa ambapo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilisema
kesi hiyo imekosa vigezo vya kisheria kutokana na kutokuwa na kibali
cha wananchi wote kwa pamoja kinachoruhusu watu nane kufungua kesi
badala ya wananchi wote.
Kama nyumba hizo zaidi ya elfu mbili
zitabomolewa basi na hizi za mwigizaji wa bongomovie Wastara zitakua
miongoni, ni nyumba ambazo anasema kiwanja chake alikinunua mwaka 2007
na gharama ya kuzijenga inazidi milioni 100 ambapo nyumba ya pili ndio
kaimalizia juzi tayari kwa kuamia.
Chapisha Maoni