HOME
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu
hatma ya suala la uchaguzi mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans
kupita muda wa kufanyika, April 25 2016 mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi wa TFF Aloyce Komba ameongea mambo matatu leo.
“Leo
kikubwa ninachotaka kukifanya kuhusu uchaguzi mkuu Yanga halafu mengine
yatafuata ni kutangaza tarehe ya uchaguzi, rasmi sasa uchaguzi wa Yanga
utafanyika June 5 2016 siku ya jumapili” >>> Aloyce Komba
“Lakini
tarehe 3 Mei 2016 nitatangaza nafasi zinazogembewa kwa mujibu wa
kalenda ya uchaguzi wa Yanga, hata hili nililolifanya la kutangaza
tarehe nilitakiwa kutangaza Mei 3 ila hiyo siku nitatangaza nafasi
zinazogombewa” >>> Aloyce Komba
“Kwa
mujibu wa katiba ya Yanga hadi sasa wanakuwa hawana uongozi na hata kama
walikuwa na kamati ya muda ina kufa na kamati yangu ndio inakuwa
inashughulikia moja kwa moja” >>> Aloyce Komba
Hayo ni baadhi ya mambo matatu
yaliotangazwa na mwenyekiti kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka
Tanzania TFF ambayepia ni wakili Aloyce Komba kuhusu uchaguzi mkuu wa
Yanga.
Chapisha Maoni