Thursday, June 19, 2014
MAKUBWA..!! NDUGU AINGIA MITINI NA RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA TYSON

Kwa mujibu wa chanzo, ndugu huyo alikabidhiwa mshiko huo kiasi cha
shilingi milioni mbili za Kibongo ambapo aliaminika kwamba baada ya
kutua Nairobi, Kenya ambako mwili wa marehemu ulipelekwa kwa mazishi
kutoka Bongo, angezikabidhi kwa familia, hasa baba na mama wa marehemu.
“Yule jamaa amefika Kenya na hakukabidhi pesa. Wengi waliamini kwamba
angezitoa baada ya kumzika marehemu kule kijijini Siaya, lakini baada
ya mazishi tu akachomoka na kurudi Nairobi.
“Mbaya zaidi amezima simu, kwa hiyo hayupo hewani. Kuna uwezekano amerejea Dar es Salaam kwa kuogopa msala wa familia,” kilisema chanzo hicho.
“Mbaya zaidi amezima simu, kwa hiyo hayupo hewani. Kuna uwezekano amerejea Dar es Salaam kwa kuogopa msala wa familia,” kilisema chanzo hicho.

Pichani
ni baadhi wa wanandugu, Monalisa na mwanaye Sonia (kulia wenye mavazi
meupe) katika msiba wa marehemu George Otieno,’Tyson’.
Kikaongeza: “Awali wakati msiba upo Dar, kuna mtu alimpa shilingi
milioni mbili akampe mama wa marehemu Kenya. Pia kuna michango mingine
iliyotolewa pale Leaders Club (Kinondoni) akakabidhiwa yeye. Na kuna
pesa ya kusafiria mtoto mmoja pia akapewa.
“Sasa baada ya kuzika tu, yule mtu aliyetoa shilingi milioni mbili
akapiga simu kwamba na yeye anakwenda msibani, ndiyo jamaa akaaga haraka
na kuondoka.
Yule alipofika akamuuliza mama wa marehemu kama alipewa shilingi milioni mbili, akasema hajapewa, kumbe jamaa aliondoka haraka kwa sababu alijua kitanuka.”
Yule alipofika akamuuliza mama wa marehemu kama alipewa shilingi milioni mbili, akasema hajapewa, kumbe jamaa aliondoka haraka kwa sababu alijua kitanuka.”
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta mdaiwa huyo kwa njia ya simu ya mkononi lakini hakuwa hewani kwa muda mrefu.
George Tyson alifariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali ya gari
akitokea Dodoma kuelekea Dar. Alizikwa Juni 14, 2014 kwenye Kijiji cha
Siaya, Kisumu, Kenya. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina
Chapisha Maoni