Wednesday, 25 June 2014
SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA KUZUIA WAKULIMA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI
Serikali imetoa ufafanunuzi kwa nini
imekuwa ikizuia wakulima kuuza mazoa yao nje ya nchi kutokana na baadhi
ya wafanyabiashara wamekuwa wakiwalangua wakulima kwa kununua mazao hayo
kwa bei ndogo tofauti na bei elekezi iliyotolewa na wizara ya kilimo
chakula na ushirika.
Naibu waziri wa fedha na uchumi Mh Adamu Malima ametoa ufafanuzi
huo Leo bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa Rombo Mh Josephu Selasini
aliyetaka kujua kwa nini serikali imekuwa ikizua wakulima kuuza mahindi
nje ya nchi ambapo wafanyabiashara wangi wamekuwa wakija nchini kununa
mahindi wengi wao wakitokea nchi jirani ya Kenya.
Mh Malima amesema kwa sasa serikali itaendelea kuzuia mahindi
kuuzwa nje ya nchi huku wizara ya kilimo chakula na ushirika ikitakiwa
kutoa bei elekezi haraka ili kuwalinda wakulima na walanguzi ambao
wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua bei ndogo na wao kwenda kuuza
bei ya juu na kunufaika zaidi ya mkulima
Chapisha Maoni