Tuesday, 15 July 2014
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MH MPESYA AFUNGUA MAFUNZO YA NISHATI ITOKANAYO NA MIONZI YA JUA KWA VIJANA
Mkuu wa wilaya ya kahama mh Benso Mpesya akifungua mafunzo hayo. |
Mkuu wa wilaya ya kahama
mkoani shinyanga Mh Benson Mpesya leo amefungua rasmi mafunzo ya nishati
itokanayo na mionzi ya jua
,yaliyoandaliwa na wakala wa nishati vijijini (REA).
Ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku saba umefanyika katika ukumbu wa
kartas wilayani Kahama mkoani shinyanga ,lengo ikiwa ni kuwapatia vijana 20
kutoka halmashauri ya Msalala ujuzi wa kufunga nishati jadilifu(solar power).
kaimu afsa elimu wilaya ya msalala SELEKA NTOBI |
Aidha mpesya amewataka
vijana kuzingatia wanayofundisha na wakufunzi pamoja na kuyaheshimu mafunzo
hayo ,kwani wakiyazingatia na kuyaelewa watakuwa wamejipatia ajira.
Kwa upande wake kaimu afisa
elimu halmashauri ya msalala Seleka
Ntobi ,amesema hiyo ni fursa kwa vijana 20 wa halmashauri hiyo kupata ujuzi
,kwani wataalamu wa ufungaji wa nishati jadilifu ni wachache katika halmashauri
hiyo.
Kupitia mafunzo hayo Seleka
ameongeza kuwa shule kumi na sita za
halmashaur ya msalala zitafungwa nishati hiyo.
Naye mkurugenzi wa ufundi kutoka kampuni ya REX ENERGY ambao ndio waendeshaji wa
mafunzo hayo Eng John Maijo ,amesema
endapo vijana hao watayazingatia mafunzo wanayopatiwa na wakufunzi
,yatawanufaisha kwani pia wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku saba
yaliyoandaliwa na wakala wa nishati vijijini (REA) na kuendeshwa na wakufunzi kutoka kampuni ya REX ENERGY kutoka Dare s salaam
yameanza leo na yatamalizika tarehe 21 mwezi huu.
mwanasemina akitoa jambo |
Chapisha Maoni