Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Japan ikotayari kutoa dawa ya Ebola   ...
HOME

Japan ikotayari kutoa dawa ya Ebola

 
Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Serikali ya Japan imesema iko tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705 ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .
Msemaji wa kampuni inayotengeneza dawa hiyo T-705 iitwayo Toyama Chemicals, anaeleza kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kukabiliana na virusi vinavyosababisha homa kali hivyo huenda ikasaidia katika mapambano dhidi ya Ebola.
Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Takao Aoki msemaji wa kampuni ambayo imetengeneza dawa hiyo, alisema kwamba dawa hiyo iliyotengenezwa ili kutibu virusi vya mafua vinavyojitokeza tena baada ya matibabu na vile visivyo vya kawaida ilipitishwa na wizara ya afya ya Japan katika mwezi wa Machi.
Akiongeza alisema kwamba Kampuni hiyo ya Fujifilm inafanya mazungumzo na utawala wa chakula na dawa Marekani juu ya kupimwa uwezo wa dawa hiyo kuhusiana na matibabu ya Ebola.
Kwa sasa hamna dawa wala chanjo yoyote iliyothibitika na kuidhinishwa kutibu Ebola, lakini kutokana na janga la mlipuko wa Ebola huko Afrika magharibi na sasa Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, Shirika la afya duniani WHO limesema itakubali matumzi ya dawa za majaribio kwa wagonjwa, ilimradi utaratibu na masharti waliyoyaweka yafuatwe na wagonjwa wenyewe wahusishwe katika kutoa idhini .
Majuzi wamarekani wawili waliokuwa wamethibishwa kuugua Ebola walipona baada ya kupewa dawa ya majaribio iitwayo ZMapp.
Daktari aliyepona Ebola baada ya kutibiwa na dawa ya Zmapp.
Yoshihide Suga ambaye ni katibu mkuu baraza la mawaziri aliwaambia wandishi wa habari kwamba Japan inawezapeana dawa hiyo wakati wowote WHO itakapoaagiza.
Aliongezea kusema kwamba Japan inangoja maelezo zaidi ya uamuzi wa WHO kuhusu matumizi ya dawa ambazo hazijajaribiwa lakini katika kesi yoyote ya dharura, Japan inaweza ikajibu maagizo yoyote ya kibinafsi hata kabla ya uamuzi wowote wa WHO.
Mapema mwezi huu WHO ilisema kwamba ni sawa kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top