Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi, Isack Kamwela akijibu swali la
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua
ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es
salaam.
Naibu
waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na
walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum)
alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo
Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akifafanua jambo Bungeni leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa Ubungo Saed Kubenea akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma
alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika
Jiji la Dar es salaam.
Silafu
Jumbe Maufi (Mbunge Viti Maalum) akiuliza swali leo Bungeni mjini
Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali iatamaliza tatizo la upungufu wa
vifaa vya kufundishia somo la TEHAMA na walimu wa masomo hayo katika
mkoa wa Rukwa.
Wabunge waliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri
wa Habari, Utaaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa na Mpiga picha
wa Gazeti la Jambo Leo Richard Mwaikenda kabla ya kuingia Bungeni leo
mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla akielekea katika ukumbi wa
Bunge leo mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilala Azzan Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini
Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Ahmed Shabiby wa Gairo
(kushoto) na Suleiman Ahmed Saddiq wa Mvomero, kwenye viwanja vya bunge
mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George
Lubeleje kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas
Gama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI
itaendelea kutekeleza ahadi zake ilizoahidi ya kuwapatia maji wananchi
wake ikiwemo wakazi wa jiji la Dar es salaam ili kutatua adha ya maji
inawakabili katika maenneo yao.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni mjini na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mahandisi Isack Kamwela wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa
Ubungo jijini Dar es salaam Saed Kubenea lenye vipengele (a), (b), na
(c) lililohoji ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika
Jiji la Dar es salaam.
Mahandisi
Kamwela amesema kuwa Serikali imekamilika na kufanikisha upatikanaji wa
maji katika jiji la Dar es salaam kwa kuongeza uzalishaji wa maji
kutoka mtambo wa Ruvu Chini na ulazaji wa bomba kubwa lenye kipenyo cha
mm 1800 kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 56.
“Hali
ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam inaendelea kuimarika
kwa kuzingatia kuongzeka kwa uzalishaji maji kutoka Ruvu Chini ambao
una uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 za maji kutoka lita milioni 180
za awali kwa siku” alisema Mahandisi Kamwela.
Katika
kuhakikisha jiji hilo linakuwa na maji ya kutosha kwa wakazi wake,
Mahandisi Kamwela amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu nao
umekamilika na una uwezo wa kutoa maji lita milioni 196 kutoka lita
milioni 82 za awali kwa siku.
Ili
kuhakikisha maji yanawafikia walengwa, Mahandisi Kamwela kazi za ulazaji
za ulazaji wa mabomba mawili kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa
tenki jipya la maji eneo la Kibamba na ukarabati wa matenki ya Kimara
zimefikia wastani wa asilimia 98, hatua hiyo imewezesha majaribio ya
uendeshaji wa mitambo hiyo kuanza mapema Aprili mwaka huu.
Aidha,
Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa
Kimbiji na Mpera ambapo hadi sasa mkandarasi amekamilisha uchimbaji wa
visima tisa kati ya visima 20 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika
mwezi Agosti mwaka huu, hadi kukamilika visima hivyo vitakuwa na uwezo
wa kuzalisha maji lita milioni 260 kwa siku.
Hadi
sasa uzalishaji wa maji katika jiji hilo umefikia lita milioni 390 kwa
siku ikilinganishwa na mahitaji ya lita milioni 450 ya sasa.
Akijibu
swali la nyongeza la Kubenea alioitaka kujua maeneo yatakayonufaika na
miradi hiyo ya maji, Mhandisi Kamwela ameyataja maeneo hayo
yatakayonufaika ni pamoja na maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo,
Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.
Maeneo
mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni
Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo,
Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama,
Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na
Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia
wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo,
Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.
Kukamilika
kwa miradi yote itaongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji katika jiji
la Dar es salaam hadi kufikia lita milioni 750 ambayo yatakidhi
mahitaji ya wakazi hao hadi kufikia mwaka 2032.
Chapisha Maoni