Unknown Unknown Author
Title: Manne aliyoyazungumza Rais Magufuli April 21 2016, wanaotumbuliwa hadharani, watumishi hewa, Bandari na CCM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME April 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na wenyeviti, makatibu wa chama c...
HOME
April 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na wenyeviti, makatibu wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ wa mikoa na wilaya za Tanzania na visiwani Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa shukrani.
Katika mambo aliyoyazungumzia Rais Magufuli ni hii ya kituo cha haki za binadamu kukosoa aina ya utumbuaji majipu hadharani kuwa ni udhalilishaji na kinyume cha sheria, hapa Rais Magufuli amelizungumzia hilo……..
>>>’wanasema tunawanyanyasa sijui haki za binadamu eti kwa sababu tunawatangaza hadharani kwa hiyo wao walikuwa na haki mno kuwaibia hadharani watanzania, waliwaibia watanzania hadharani lazima tuwatangaze hadharani, mateso waliyoyapata watanzania mamilioni kwa sababu za kuibiwa na hawa wachache lazima na wao waanze kupata hayo mateso’:-Rais Magufuli
>>’kwa hiyo unaweza kuona hawa wanaowatetea nao ni majipu nao tutaanza kuwafuatilia, lakini kwa bahati nzuri aliyewateua ni mimi na niliwataja hadharani kwa hiyo kwa nini wafurahi siku ya kuteuliwa na wasitajwe hadharani siku ya kutumbuliwa’:-Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli ameligusia suala la watumishi hewa……..>>>’mpaka leo wafanyakazi hewa tuliowatoa kwenye register wamezidi 7700 na bado uchambuzi unaendelea sasa mnaweza mkaona kama kuna wafanyakazi hewa wa namna hiyo ndani ya serikali, hayo mabilioni ya fedha yangeweza kwenda kwenye huduma mbalimbali;-Rais Magufuli
Ameligusia pia suala la stori zilizoenea kuwa mizigo imepungua bandarini kwa sasa…….>>>’iliyopungua ni ya wale waliokuwa wanaingia bila kulipa kodi, na wale waliokuwa hawalipi kodi wasije, nafuu uwe na mizigo michache ya watu walio commited kulipa kodi‘:-Rais Magufuli
>>>’nataka kuwahakikishia ndungu zangu wana CCM nchi itakwenda na bahati nzuri sasa hivi tumeanza kupata support kubwa sana kwa wafadhili hakuna mfadhili anayependa watu wa kwao huko walipe kodi halafu nyie mzitumie vibaya, baada ya hatua hizi tulizozichukua kila mmoja anasema analeta fedha’:-Rais Magufuli
Rais Magufuli akamalizia kwa kuwaomba viongozi wa CCM kusahau yaliyopita na kuwa pamoja>>>’niwaombe tu viongozi wenzangu wa chama cha mapinduzi kwa sababu sasa hivi kampeni zimeisha na nimesema yaliyopita sio ndwele, tulifikia mahali kwa kutoaminiana na tukishajenga tendecy ya namna hiyo tutakuwa tunakiua chama’:-Rais Magufuli
1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wenyeviti, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na Wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam
2 Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
3Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kulia kwake ni makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti CCM Taifa Philip Mangula na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani Ikulu jijini Dar es Salaam
3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa Ikulu jijini Dar es Salaam
4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini mara baada ya kumaliza kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top