Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Huduma ya dharura kwa watumishi wa umma Kenya imeboreshwa, kumeletwa ndege ambazo ni ambulance mtu wangu! ...
HOME

Huduma ya dharura kwa watumishi wa umma Kenya imeboreshwa, kumeletwa ndege ambazo ni ambulance mtu wangu!

150114163803_president_kenyatta_1Vifaa vya uokoaji ni vitu muhimu katika jamii hasa pale matatizo yanapotokea, ni  vizuri msaada ukapatikana mapema pale ambapo unahitajika, Serikali ya Kenya imeamua kufanya hili kama moja ya njia za kuboresha huduma ya dharura kwa watumishi wa umma.
Tumesikia malalamiko mengi kutoka kwa watumishi wa Serikali kuhusu huduma kuwa si za kuridhisha mbali na kuwa wanakatwa kodi kubwa kwenye mishahara yao kila mwezi.
Kenya wamezindua huduma za dharura kwa kutumia ndege na magari ya kisasa kwa watumishi wa umma, uzinduzi wa huduma hiyo ulihudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Huduma hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano na Shirika la Bima ya Afya, Shirika la Msalaba Mwekundu na kundi la madaktari wanaosafiri kwa ndege la AMREF.
Huduma hiyo inafanya Kenya kuwa nchi ya pili baada ya Afrika Kusini kutoa huduma ya aina hii, inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wanajeshi ambao wanapigana vita katika maeneo mbalimbali yaliyopo mbali na maeneo yenye huduma za afya.
150114163803_president_kenyatta_3
.
Rais Uhuru Kenyatta akipewa maelekezo namna gari ya dharura inavyofanya kazi.
.
Rais Kenyatta akipewa maelekezo namna huduma inavyotolewa ndani ya ndege.
150114163803_president_kenyatta_1
Hapa unaweza kuona namna ambavyo AMREF wameuwa wakifanya shughuli zao za uokoaji.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top