HOME
Majibu ya Utafiti kuhusu watu wazima wanaokojoa kitandani Tz…
Kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano kukojoa kitandani au
kujikojolea ni jambo la kawaida, lakini vijana na watu wazima
kujikojolea kitandani mara kwa mara siyo jambo la kawaida katika jamii.
Kitabu cha afya ya akili kilichotolewa
na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya akili cha Marekani kinasema kuwa
kikojozi ni mtu mwenye tatizo la kujikojolea nguoni au kitandani angalau
mara mbili kwa wiki kwa muda wa miezi mitatu mfufulizo akiwa na umri wa
miaka mitano au zaidi.
Tafiti zinaonyesha kwamba katika kila
watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi na kwa upande wa Tanzania, hivyo
inayokadiriwa kuwa na Watanzania milioni 50 idadi ya watu wazima
vikojozi inakadiriwa kuwa ni sawa na nusu milioni.
Wengine wanahusisha tatizo hili na
matatizo ya mishipa ya fahamu kushindwa kumpatia muhusika taarifa ya
kujaa kwa kibofu pindi anapokuwa usingizini na sababu nyingine ni uwezo
mdogo wa kibofu kushindwa kubeba mkojo wa kutosha kutokana na kulegea
kwa valvu zake.
Sababu za tatizo hili ni pamoja na kukomaa kwa tezi ya pituitary
inayopatikana ndani ya ubongo ambapo ikikomaa husababisha figo
kuzalisha kiasi kikubwa cha mkojo na matokeo yake muhusika akiwa
usingizini hupoteza uwezo wa kuudhibiti.
Chanzo cha story: Gazeti la Mwananchi, Toleo la January 16, 2015.
Chapisha Maoni