HOME
Na. Catherine Sungura.
Wazazi
nchini wametakiwa kuwakinga watoto wao wakati waendeshapo magari kwa
kuhakikisha wanawafunga mikanda ili kuwaepusha na ajali za barabarani na
kudhibiti madhara yatokanayo na ajali.
Rai
hiyo imetolewa leo jijini hapa na kaimu kamanda kikosi cha usalama
barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus
Musilimu wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili,Mahakimu ,Waendesha
Mashitaka na Askari wapelelezi wa kesi za ajali za
barabarani,iliyoandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika
la Afya Duniani (WHO) kupitia mpango wa Bloomberg Initiative Global Road
Safety.
Alisema
wazazi wengi wanapokuwa wanaendesha magari hawawafungi mikanda watoto
wao na hivyo ajali inapotokea watoto wanakuwa ni wahanga wakubwa kwa
kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu
“Wazazi
mnawalindaje watoto,baba anaendesha gari,mtoto yupo kwenye usukani
anaendesha nae gari,hiyo siyo sahihi ,tuwalinde watoto wawe salama kwa
kuvaa mikanda”
Aidha,
Kamanda Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani nchini imekua
ikiongezeka kila mwaka na hii ni kutokana na wananchi kutokuona kama
ajali ni tatizo kubwa na la haraka ambalo linafanya kuongezeka kwa vifo
nchini kulinganisha na magonjwa mengine na hivyo kupoteza nguvu kazi ya
taifa kiuchumi.
“Watu
bado hawaoni kama ajali ni tatizo ,vifo inatokea hapohapo na watoto
wanabaki kuwa tegemezi,hizi ni changamoto hivyo mshirikiane
kubadilishana uzoefu ili muweze kutatua kesi zote zinazowafikia na
kupunguza malalamiko pamoja na kutenda haki,alisema.
Takwimu
za hapa nchini kwa miaka miwili zinaonesha mwaka 2014 zilitokea ajali
14,360,vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015 zilitokea ajali
8,337,vifo 3,468 na majeruhi 9,383,hata hivyo Ripoti ya Shirika la Afya
Duniani ya mwaka 2015 zinaonesha ajali huua watu 1.25 milioni Duniani
kila mwaka, watu kati ya 20 na 50 milioni hujeruhuwa kila mwaka na
hivyo asilimia 90 ya ajali hizi na vifo hutokea katika nchi zenye
uchumi wa kati na wa chini kama Tanzania.
Kamanda
Musilimu alisema kasi hii ya ajali ikiendelea hadi ifikapo mwaka
2030,ajali itashika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo Duniani.
Mradi
wa Bloomberg Initiatives ni mradi wa miaka mitano hapa nchini
umeanzishwa mwaka 2015 ukiwa na nia ya kuweka vipaumbele vya kuzuia
vyanzo vya ajali hatarishi kama vile mwendo kasi,kutokuvaa kofia
ngumu,kutokufunga mikanda,vifaa maalumu vya kuwakinga watoto kwenye
magari pamoja na ulevi.
Chapisha Maoni