Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza
wabunge kwa kushiriki vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na
kurudi salama mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi hizo za Spika zimetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson
kwa niaba ya Spika alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge
hadi jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya
Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George
Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.
Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni
timu za mpira wa miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa
kuishinda timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15 wakati
timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1
Kushiriki kwa Wabunge katika mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo
kati ya pande mbili za Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili
ya kujenga na kuimarisha afya zao.
Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo
cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi
mbalimbali katika kujenga na kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani
mwema.
Ushiriki wa Wabunge kwenye mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki
michezo mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za
Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo yaliyoendeshwa na
klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini Unguja kwa kuzingatia Bunge
lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi mazoezi ya viungo (Gym).
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mbunge
wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja
wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na
Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati
kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na
Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella
Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Wabunge
wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na
Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa
Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika picha
ya pamoja na wageni wake waliomtembelea leo Bungeni, mjini Dodoma.
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Bungeni,
mjini Dodoma. (Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma).
Chapisha Maoni