HOME
WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA WATOTO 3 WAKAMATWA KAHAMA
Afisa wa uhamiaji akichukuwa maelezo kwa muhamiaji haramu Tengemea Benjamini ofisi za uhamiaji
Wahamiaji haramu
kumi na watoto watatu wamekamatwa wilayani kahama mkoani shinyanga wakiwa wakielekea
mkoani tabora kwenye mashamba ya tumbaku kwa ajili ya kilimo.
Haya aliyesema
hayo jana kamishana wa Uhamiaji Wilaya
ya Kahama Zakari misana wakati akizungumza na redio kyela fm ofisini kwake
ambapo alisema kuwa wahamiaji hao walikamatwa katika kituo cha mabasi wakati
wakimsubiri mwenyeji wao ili kuwapeleka mkoani tabora.
Alisema kuwa
wahamiaji hao ambao ni Rai wa nchi jamhuri ya Burundi waliangizwa na mkazi moja
wa Tabora ambaye aliyejulikana kwa jina
moja la shabani,ambapo baada ya kukamatwa na kupata taarifa ndipo wenyeji wao
walipokimbia kutojulikana.
Misana aliwataja
wahamiaji hao kuwa ni Emily Havyarinana(33),Habimana paschal(45),masabo Tadei(
34),Bahati leopoo( 42),Niondeze John(24),Emmanuel mathayo( 21),Tegemea
Benjamini( 23) mkazi wa chivu ,joseph Elias (12), ,Laneck wilford (17),Estar
John (18) raia wa Burundi pamoja na Irene stephe(20)raia wa Tanzania mkazi wa ngara.
Aidha Misana
alisema kuwa walikuwa wanakwenda Mkoani Tabora katika kijiji cha Isakamleme kwa
ajili ya shughuli za kuvuna mahindi, kuchambua Tumbaku pamoja na kuvuna mpunga.
Katika hatua
nyingine alisema kuwa Irene Staphano ameajili mtoto mwenye umri wa miaka(8) aliyejulikana
kwa jina moja la Khadija mkazi wa Burundi jambo ambalo ni kosa kuajili mtoto
mdogo ambapo ni kinyume cha sheria ya jamhuri ya Muungano waTanzania.
Misana alisema
miezi kama hii katika mikoa ya mipakani
kumekuwa na tatizo la wahamiaji haramu wanaokimbilia mikoa ya kagera,Tabora pamoja
na shinyanga, ambapo wilaya ya kahama imejipanga vyema katika kamati ya ulinzi ili
kudhibiti jambo hilo.
Misana aliwataka
watendaji wa kata na vijiji vilivyopo
mipakani kushirikiana na wananchi kudhibiti matatizo ya wahamiaji hao ambapo
amesema kuwa atakayebainika kuishi na raia ambaye sio raia ya Tanznia
atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ambapo alisema
kuwa wahamiaji hao watachukuliwa hatua za kisheria baada ya kuingia nchini bila
kibali hivyo watafikishwa mahakamani wilayani humo ili kujibu kesi inayowakabili.
MATUKIO KATIKA PICHA.
IRene mkazi wa ngara ambaye moja wa
tanzania ambaye anajiushisha na kukaa na wahamiaji haramu na mtoto
khadija 8 miaka ambaye ni Raia wa Burundi anayefanya naye kazi kwake.
Baadhi ya wahamiaji wakiwa chini ya ulinzi katika ofisi za uhamiaji kahama baada ya kukamatwa.
Mtoto khadija akiwa na mtoto wa Ireni stephen ambaye amembeba kwa ajili ya kumlea mtoto huyo.
Irene akiwa na watoto wake wawili na mfanyakazi wake wa watoto wake khadija ofisi ya uhamiaji kahama kwa mahojiano.
Irene akiwa na afisa wa kike ofisi za uhamiaji kahama na watoto wake baada ya kukamatwa kituo cha mabasi.
Irene akihojiwa na kamishina wa
uhamiaji Zakaria Misana ofisi kwake kwa kosa la kukaa na mtoto wa miaka 8
kumfanyisha kazi kinyume na sheria.
Kamishina wa uhamiaji zakari misana akiongea na waandishi wa habari ambao wapo picha juu ya wahamiaji haramu ofisini kwake .
Wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji kwa kosa la kuingia nchini bila kibali
Afisa wa uhamiaji akifanya mahojiano na moja wa wahamiaji haramu ofisi za uhamiaji .
Chapisha Maoni