HOME
NA GORDON KALULUNGA
Kwa umuhimu na ommbi la baadhi ya wasomaji kuomba makala hii irudiwe kuchapishwa, hatuna budi kuirejea tena. Endelea kusoma.
NIANZE kwa kuwapa pole watanzania popote pale walipo hasa wale ambao wamepatwa na maafa na adha zingine zilizotokana na mvua zinazoendelea kunyesha tangu mwaka huu uanze.
Wiki hili ni wiki la kuzigusa siku 100 za Rais Dkt. John Magufuli
tangu achaguliwe na kuapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwasisi wa dhana ya siku 100 madarakani tunaambiwa kuwa ni aliyekuwa Rais wa Marekani wa 32, Franklin Roosevelt, ambaye alichukua madaraka ya nchi hiyo ikiwa imeyumba kiuchumi na umma kupoteza imani kwa serikali.
Hakuna ubishi kuwa Rais Magufuli aliichukua nchi kutoka kwa mtangulizi wake, mwanadiplomasia mbobezi, msuluhishi wa kimataifa, Rais mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, umma ukiwa umepoteza imani kwa serikali kwa kiwango kikubwa.
Ndani ya siku 100 za utawala wa Rais Magufuli, licha ya kuwaudhi
baadhi ya watanzania wakiwemo (majizi), ndani ya serikali na sekta
binafsi, amejitahidi kuwa mlezi na mlinzi mithili ya ndege aina ya
Hondohondo.
Kuna ndege huku kwetu nyikani anaoitwa Hondohondo, wengine humwita lilikuliku. Kichwa ni kikubwa kuliko mwili na mdomo wake mrefu, mbaya sana kwa sura. Kila akiruka huonekana anapepesuka, nadhani kwa kulemewa uzito wa kichwa.
Lakini Hondohondo ana sifa moja kubwa sana. Anawapenda wanawe kupindukia, na hodari wa kulea. Maisha yako hutapata kuokota kinda lake likiwa hai, labda likiwa limekufa.
Watu humsifia sana ndege aina ya Chiriku. Kwa kweli ni ndege mzuri sana wa umbo, tena mwingi wa ujanja na maneno. Chiriku hutaga mayai mengi na hupata makinda mengi sana, lakini wanaokua ni wachache tu.
Kwa sababu akishatotoa, huruka na kuwaacha makinda kisha yeye huruka na kwenda kupiga domo.
Ndiyo maana si ajabu kuokota makinda ya Chiriku barabarani maana, yanaachwa peke yao na yale yanayojitahidi kuruka na kuangaka ndiyo huokotwa. Hondohondo au Lilikuliku si hivyo.
Wakati akitotoa, naye hujinyonyoa manyoya yote, yeye na makinda yake wanakuwa katika hali sawa kabisa, isipokuwa mdomo tu.
Manyoya yakianza kuota, yanaota pamoja na mama akiwafunza watoto wake kuruka huwafunza kidogo kidogo sana, maana hata yeye uwezo wa kuruka mbali hana. Lakini kanjinyang’anya uwezo huo mwenyewe kwa kuwapenda wanawe.
Naye atakuwa na wanawe akifunza mambo kidogo kidogo mpaka hapo watakapopata uwezo wa kujitegemea.
Ndege huyo hatagi mayai mengi, lakini hao watoto wachache atakaototoa, wote watakua na kama wakipatikana na dharura basi ni kwa bahati mbaya kabisa maana mwenyewe haondoki kwa wanawe mpaka wamekua kabisa.
Mfano huo wa ndege Hondohondo na Chiriku unasadifu na viongozi wetu kadhalika. Tunao viongozi maelfu, katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Na uongozi ni ulezi. Basi wako wale wenye kupendeza sana umbo na maneno matamu yenye kupendeza watu. Lakini ulezi wao kama wa Chiriku, ni uongozi wa maneno.
Miaka nenda rudi wananchi wamekuwa wakilalama kila kukicha kuhusu matatizo yanayowakabili, lakini viongozi na watumishi wa umma mithiri ya Chiriku, wamekuwa wakifumbia macho.
Mfano barabara ya kutoka Mpemba kwenda Isongole wilayani Ileje mkoani Mbeya (Songwe kwa sasa) ni mbaya sana, imekuwa barabara ya kuombea kura kwa watawala. Jambo hili si la kufumbiwa macho na watawala mithili ya Hondohondo, bali Chiriku tu.
Watu wa nyikani tunaweza kuchambua kuwa, Rais Dr. Magufuli ana ulezi wa Hondohondo, tangu atangazwe na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hajaweza kusafiri kwenda nje ya nchi. Ameamua kulea kwanza vifaranga vyake mpaka hapo atakapoona vifaranga vimeanza kuwa na uwezo wa kujitegemea. Ameanza vema na siku 100 za uongozi wake. Kuna changamoto kadhaa zinazolikabili (tukabili) Taifa, sote
tunahusika kuzitatua kwa kufanya kazi na kubuni kazi za kuzifanya hasa vijana walioko Vijijini na mijini.
Hapa tulipofikia, tunahitaji viongozi aina ya ndege Hondohondo kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa. Viongozi wanaokubali kujinyonyoa, wakajishusha hali zao kwa ajili ya kuwalea wengine.
Shida nyingi za mjini ni wizi kwenye sekta za umma, viburi na kutumia madaraka vibaya.
Shida kubwa za vijijini ni miundombinu ya barabara, maji, fursa za vibarua (ajira), uhaba wa watumishi, miti ipo vijijini lakini wanafunzi hawana madawati, watumishi wa umma kufanya kazi kwa mazoea, masoko ya mazao ya wakulima na ubabe wa baadhi ya watendaji wa Vijiji na kata.
Kiongozi aliyezoea kuishi mjini kwenye barabara za lami, Maghorofa, maji ya bomba, kutembelea magari hawezi kusikia sawa sawa sauti hii ya watu wa nyikani.
Hitimisho
kwa tathimini ya sauti hii ya nyikani, kuhusu siku 100 za Rais
Magufuli tangu awe Rais wa Tanzania mwaka jana 2015, ameanza vema na ameonyesha tumaini kuu kwa watanzania wanyonge na kuanza kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao huku ikianza kuonekana nuru ya dhana ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayoipambanua Tanzania kuwa ni nchi ya ujamaa na kujitegemea, ambayo ilifichwa gizani.
Uongozi wa kijamaa unajali binadamu wengine. Ninaamini kuwa Dr. Magufuli ni mmoja kati ya wajamaa ambao wamebakia ndani ya CCM na miongozi mwa watanzania, ambao hawasubiri wakati tu ule wa uchaguzi kwa ajili ya kuomba kura.
Tumtakie kila la kheri katika utawala wake Rais Magufuli huku
tukiwatazama ndege wawili yaani Hondohondo na Chiriku ili ikifika
mwaka 2019-2020, tuje tuwalipe walichopanda.
Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa simu 0754 440 749 na barua pepe ni kalulunga2006@gmail.com

Chapisha Maoni