Jumamosi21/06/2014
AJALI MBAYA ILIYOTOKEA KWENYE DARAJA LA MTO NDURUMA – ARUSHA
Mashuhuda wa ajali na baadhi ya gari ziliwa kwenye foleni baada ya kushindwa kuendelea na safari.
Baadhi ya gari zikipita barabara ya fumbi ili kukwepa foleni iliyosababishwa na ajali hiyo.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ambavyo foleni ilikuwa ikiongezeka na watu walizidi kufurika katika eneo la ajali.
ARUSHA
Jana majira ya saa tisa alasiri ilitokea ajali mbaya katika daraja la
mto nduruma lililopo eneo la kambi ya chupa Madukani, wilaya ya Arumeru
jijini Arusha. Ajali hiyo ilisababisha kukatika kwa mawasiliano
mawasiliano ya pande mbili kati ya abiria/watu waliokuwa wakitokea
upande wa Arusha mjini wakielekea upande wa tengeru, user river, Kia
mpaka Moshi na wale abiria/watu waliokuwa wakielekea Arusha mjini.
Ajali
hiyo iliyosababishwa na semi trailer iliyokuwa ikitokea Arusha kufeli
breki na kuyapanda matuta kwa mwendo wa kasi jambo lililopelekea dereva
wa semi traler kushindwa kulihimidi gari na kugongana uso kwa uso na
lori iliyokuwa ikielekea upande wa Arusha mjini. Ajali hiyo ilisababisha
foleni kubwa sana iliyopelekea adha kwa wasafiri waliokuwa wakiitumia
barabara hiyo pamoja na daraja la mto nduruma.
Foleni ilikuwa kubwa sana kiasi ambacho ilibidi baadhi ya wasafiri waliokuwa wakitokea Arusha wakielekea upande wa Moshi kuamua kupita baraba ya mashono moivaro na kwenda kutokea tengeru na wengine walitokea user river, ambapo kwa magari makubwa haikuwa rahisi kufanya hivyo. Na mpaka sasa hakuna yeyote aliyefariki kutokana na ajali hiyo ila inasemekeana dereva aliyekuwa anaendesha lori anahali mbaya sana. Madereva wawili waliokuwa kwenye semi trailer walitokomea kusiko julikana na mpaka sasa hawafahamiki walipo kimbilia.
Mtandao huu ulipojaribu kuwauliza baadhi ya madereva wanaoitumia barabara ya Arusha mpaka Moshi kuhusu ajali zinazotokea kwenye daraja la mto nduruma walisema uwepo wa matuta hayo kwenye eneo la daraja la mto nduruma kuwa ndio chanzo cha ajali, lakini wengine walikanusha na kusema matuta hayo yamekuwa yakiwalazimisha madereva kupunguza mwendo kasi na kupunguza uwezekano wa kupata ajali.

Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.