HOME
April 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli
amekutana na wenyeviti, makatibu wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ wa mikoa
na wilaya za Tanzania na visiwani Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili
ya kutoa shukrani.
Katika
mambo aliyoyazungumzia Rais Magufuli ni hii ya kituo cha haki za
binadamu kukosoa aina ya utumbuaji majipu hadharani kuwa ni
udhalilishaji na kinyume cha sheria, hapa Rais Magufuli amelizungumzia hilo……..
>>>’wanasema
tunawanyanyasa sijui haki za binadamu eti kwa sababu tunawatangaza
hadharani kwa hiyo wao walikuwa na haki mno kuwaibia hadharani
watanzania, waliwaibia watanzania hadharani lazima tuwatangaze
hadharani, mateso waliyoyapata watanzania mamilioni kwa sababu za
kuibiwa na hawa wachache lazima na wao waanze kupata hayo mateso’:-Rais Magufuli
>>’kwa
hiyo unaweza kuona hawa wanaowatetea nao ni majipu nao tutaanza
kuwafuatilia, lakini kwa bahati nzuri aliyewateua ni mimi na niliwataja
hadharani kwa hiyo kwa nini wafurahi siku ya kuteuliwa na wasitajwe
hadharani siku ya kutumbuliwa’:-Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli ameligusia suala la watumishi hewa……..>>>’mpaka
leo wafanyakazi hewa tuliowatoa kwenye register wamezidi 7700 na bado
uchambuzi unaendelea sasa mnaweza mkaona kama kuna wafanyakazi hewa wa
namna hiyo ndani ya serikali, hayo mabilioni ya fedha yangeweza kwenda
kwenye huduma mbalimbali;-Rais Magufuli
Ameligusia pia suala la stori zilizoenea kuwa mizigo imepungua bandarini kwa sasa…….>>>’iliyopungua
ni ya wale waliokuwa wanaingia bila kulipa kodi, na wale waliokuwa
hawalipi kodi wasije, nafuu uwe na mizigo michache ya watu walio
commited kulipa kodi‘:-Rais Magufuli
>>>’nataka
kuwahakikishia ndungu zangu wana CCM nchi itakwenda na bahati nzuri
sasa hivi tumeanza kupata support kubwa sana kwa wafadhili hakuna
mfadhili anayependa watu wa kwao huko walipe kodi halafu nyie mzitumie
vibaya, baada ya hatua hizi tulizozichukua kila mmoja anasema analeta
fedha’:-Rais Magufuli
Rais Magufuli akamalizia kwa kuwaomba viongozi wa CCM kusahau yaliyopita na kuwa pamoja>>>’niwaombe
tu viongozi wenzangu wa chama cha mapinduzi kwa sababu sasa hivi
kampeni zimeisha na nimesema yaliyopita sio ndwele, tulifikia mahali kwa
kutoaminiana na tukishajenga tendecy ya namna hiyo tutakuwa tunakiua
chama’:-Rais Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia Wenyeviti, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na
Wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wenyeviti na
Makatibu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kulia kwake ni makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti CCM Taifa Philip Mangula na
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani Ikulu
jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa Ikulu jijini
Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mikoa
mbalimbali nchini mara baada ya kumaliza kuzungumza nao Ikulu jijini Dar
es Salaam
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.