MAKALA
MIAKA mingi iliyopita ilikuwa si kawaida kumwona msichana au mwanamke
akiendesha gari, au akijiingiza kwenye ufundi na masuala ya maarifa;
alipoonekana watu walishangaa lakini kutokana na mabadiliko ya sayansi
na teknolojia, hicho sasa ni kitu cha kawaida katika nchi zilizoendelea.
Safari ndefu huanza kwa hatua ya kwanza, na Waswahili husema kwamba hakuna mawaridi pasipo kwanza kupitia miiba, ndiyo maana jitihada za kumkuza mwanamke kielimu zimekuwa zenye matatizo makubwa. Binafsi hujiona salama zaidi ninapoona rubani mwanamke ameshika hatamu kwenye ndege, na katika umakini wao, wanawake wakipewa nafasi wanaweza kuja kuwa mahiri sana katika sayansi na teknolojia.
Kuwapo wanaume wengi katika kushikilia gurudumu la teknolojia na ufundi hakumaanishi hata kidogo kwamba eti wanawake hawawezi; kinyume chake ni kielelezo na mfano anuai wa jinsi wanawake wanavyobinywa na kunyimwa haki yao hiyo. Katika karne ya 21 inasikitisha kuona kwamba Tanzania haiwaandai vilivyo watoto wa kike kuwa marubani wetu wa siku zijazo, kwenda kwenye mwezi au sayari nyingine kutafiti.
Hali ni hiyo kwa sababu msingi wa yote hayo ulitakiwa uwe kuanzia elimu ya msingi, sekondari na kuendelea. Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unaonesha kwamba maarifa hayo yatakuwa vigumu kufikiwa, kwa sababu kielimu ufaulu wa watoto, hasa wa kike, unashuka hata kama kuna kujigamba hapa na pale kwamba watu wengi wamefaulu.
“Ufaulu wa mitihani ya darasa la saba umeshuka kwa jumla lakini wasichana wanafanya vibaya kuliko wavulana. Ufaulu ulishuka toka asilimia 70.5 mwaka 2006, hadi kufikia asilimia 54.2, kisha 52.7% hadi 49.4% kwa miaka ya 2007, 2008, 2009,” anasema Profesa Ruth Meena.
Kwa msingi huo, wasichana wengi wataishia njiani tu, na kana kwamba hiyo haitoshi, takwimu za mwaka 2009 zinaonesha kwamba asilimia 56.7 % ya wanafunzi walioshindwa walikuwa wasichana. “Wasichana wasiomaliza masomo ya sekondari wanaongezeka. Mwaka 2010, kiasi cha wanafunzi wa shule za sekondari ambao hawakumaliza masomo yao walikuwa 31,144.
Kati yao wasichana wakiwa 19,619 na wavulana 11,522 sababu za kutokumaliza masomo ni utoro kwa asilimia 36.2% ikifuatwa na mimba kwa kadiri ya asilimia 20.4,” anaeleza msomi huyo. Ingawaje ufikiaji wa elimu kwa wasichana umeongezeka katika ngazi zote za elimu, bado wasichana ni wachache kuliko wavulana na hilo linadhihirishwa na takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zilizotolewa mwaka 2012.
Profesa Meena ambaye ni Mwanaharakati wa Jinsia na Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kwamba ufaulu wa wanafunzi wa sekondari kwa wasichana na wavulana umekuwa ukishuka kutoka asili mia 16 mwaka 2001, hadi zaidi ya asilimia 50 mwaka 2010.
Kwamba mwaka 2011 kumi bora kwenye ufaulu walikuwa wasichana, lakini ukiangalia kwa jicho la maarifa kwa wastani ni kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi ya wavulana. Haina maana sana kusherehekea na kufurahia vichwa vya habari kwamba wasichana wamewakaba wavulana wakati kiuchambuzi wa kitaalamu si hivyo.
TGNP inabainisha katika utafiti wake kwamba kati ya watahiniwa 458,114 waliofanya mitihani ya kidato cha nne, wavulana 27,805 walipata daraja la 1-111 hivyo kuwawezesha kupata nafasi za kuingia kidato cha tano. Hata hivyo, wasichana waliofaulu kwa madaraja hayo ni 12,583 tu. Idadi ya wavulana waliopata sifuri ni 83,150 na wasichana ni 91,043.
Tofauti hiyo ni kubwa, na msisitizo wa hali ya juu unapaswa kuwekwa katika kuwezesha wasichana kufanya vizuri, na hili litafanikiwa ikiwa uhamasishaji, uwezeshaji na ukubali kutoka serikalini, taasisi na idara zake, mashirika ya umma na ya kiraia kufanya kazi pamoja. Katika mwaka 2013, ufaulu kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ulishuka, kwani waliofeli walifikia asilimia 62 ikilinganishwa na asilimia 46 ya mwaka 2011.
Ina maana waliokwenda kidato cha tano ni asilimia ndogo zaidi. Kwa jinsi hii, Profesa Meena anahoji lini Tanzania itaona wanawake wengi zaidi wakiwa katika nafasi nyeti kisayansi na teknolojia pamoja na maarifa? Yaweza kuwa ndoto kama jitihada za pamoja hazitafanywa.
Mambo hayaishii hapo, kwa sababu ili kuweza kurusha ndege, kumudu mashine kubwa kubwa na za kisasa kwenye dunia ya sayansi na teknolojia elimu ya juu ni lazima. Lakini utafiti unaonesha kwamba udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2010/11 ulikuwa jumla ya wanafunzi 139,638 wanawake wakiwa ni 49,959, idadi hii iliyongezeka kufikia 166,484 (wanawake 60,592) katika mwaka wa masomo uliofuata.
Wakati tunasema elimu ni ufunguo wa maisha, kazi ni msingi wa maisha na maendeleo huletwa na kazi kama tulivyofunzwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuna ukweli mwingine unaopewa kisogo. Lillian Liundi ni Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, anakuja na hoja kwamba bila afya njema, hayo yote ya elimu na kazi hayawezekani, kwa sababu afya ndio msingi wake yote.
Na suala la afya ni tete, kwani linahitaji teknolojia ya hali ya juu. Liundi anasema wanawake wanaweza kuvuka vihunzi ikiwa watajengewa mazingira mazuri tangu mapema na wakiwa shuleni na kwamba tafiti nyingi zilizofanywa zinaonesha kuwa wasichana wanapoandaliwa mazingira mazuri ya elimu wanafanya vizuri ukilinganisha na wavulana.
Ushahidi wa hayo ni juu ya shule zinazochukua wasichana pekee ambazo zimekuwa zikifanya vizuri zaidi jambo ambalo linaonesha wazi mazingira mazuri yakijengwa jamii hii inaweza kuinuka na kuwa mfano mzuri. Lakini je, ni wangapi wanahakikishiwa afya kwa nchi yetu kukumbatia teknolojia mwafaka kwa watu wake?
Na swali muhimu nzaidi, kwa nini tujenge hoja ya ktetea haki ya afya ya uzazi kubainishwa katika katiba mpya? Liundi anasema, afya ambayo ni msingi wa maisha, inaanzia kwenye afya ya uzazi na elimu na haki ya uzazi salama ambayo ndiyo chanzo cha uhai, ikimaanisha lazima mtoto wa kike aangaliwe tangu mapema kabisa kabla hajafikia ujana.
Maarifa lazima yatolewe kwa watoto wa kike na wengine wote juu ya afya ya uzazi kwa sababu ni muhimu kwa taifa, kwani wanawake wanapokuwa na afya na usalama wa maisha yao, watazaa watoto wenye afya, na hivyo kuwezesha taifa kuwa na rasilimali watu wenye afya.
Hata hivyo, Liundi anasema kwamba mambo yamekuwa tofauti, na inasikitisha katika karne hii ya sayansi na teknolojia, tunaendelea kushuhudia vifo vya wanawake katika uzazi, jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki yao ya kuishi, na vile vile ni gharama kwa taifa. “Tanzania ipo juu kwenye idadi ya wanawake wanaokufa kutokana na vifo vya uzazi.
Takribani wanawake 460 kati ya kila wanawake 100,000 wanaojifungua hupoteza maisha yao, idadi hii huweza kubadilika kati ya 190 hadi 740,” anasema mwanaharakati huyo. TGNP inaona kwamba wasichana wenye umri mdogo wanapata changamoto nyingi za kiafya, jambo linaloashiria kuhatarisha maisha yao.
Hata hivyo huduma nyingi za afya za jamii si rafiki kwa watoto wa kike, hivyo jambo hili linatakiwa kuingizwa kwenye katiba mpya. Liundi anasema mengi yanayowakumba wanawake ni kutokana na ama ukosefu wa maarifa, teknolojia au vifaa takikana kwenye hospitali, ikiwa ni pamoja na maabara zisizokuwa na vifaa au wagonjwa na ndugu zao kutakiwa kupeleka vifaa.
Ukosefu wa huduma, hususani elimu ya uzazi kwa vijana huashiria kuhatarisha maisha wa watoto wa kike na ieleweke kwamba takribani nusu ya Watanzania ni vijana chini ya umri wa miaka 18.
“Takribani nusu ya wasichana wenye umri chini ya miaka 19 wamepata ujauzito au tayari wana watoto. Takribani mmoja kati ya wasichana watatu (28%) wenye umri kati ya miaka 15-19 kutoka kaya maskini wameshaanza kuzaa. Tanzania inaongoza duniani kwa mimba za watoto wadogo wa kike,” anasema Liundi.
Anabainisha kwamba taarifa za Takwimu za Utafiti wa Afya Tanzania (TDHS) za mwaka 2010, zinaonesha kwamba, asilimia 23% ya wasichana wenye umri mdogo wameshakuwa na watoto na vilevile asilimia 14% ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi ni wasichana kati ya miaka 15-19.
Lakini pia, taarifa za karibuni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) zinaonesha kwamba Tanzania inaongoza duniani kwa idadi ya mimba za watoto wadogo. Kwamba karibu wasichana wawili kati ya watano huwa wameshaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Na takribani asilimia 37 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 walishaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Katika mazingira hayo, wanawake hawa watawezaje kufikia ndoto kubwa walizokuwa nazo tangu wakiwa watoto, walipokuwa wanakua kwamba siku moja nao waje kuwa madaktari, wabobee kwenye upasuaji, wawe makanika, mafundi kwenye sekta mbalimbali na hata marubani?
Liundi anasema ndoto zote hizo zinafutwa na kutoangaliwa vyema kwa watoto wa kike na kutowekwa katika mazingira ya kulishwa maarifa ili hatimaye taifa lije kujidai kuwa juu kiteknolojia. Usione vyaelea kwa wengine, vimeundwa, anahitimisha.
Wanawake wanavyonyimwa maarifa kwa sababu ya jinsia.

Chapisha Maoni