HOME
Makala
Lini wakulima wa Tanzania watasaidiwa wafurahie kilimo?
Baadhi ya waliokimbia kilimo wanasema kwa namna
inavyoonekana hakuna mpango wa maana katika kusaidia kilimo nchini.
Badala yake wanasiasa wanawatumia wakulima kama mtaji wakati wa kampeni
kwa kuwapa ahadi za misaada
“Kuna pembejeo, kuna uuzaji ghalani, lakini
Serikali haisimamii vizuri, haijali malalamiko ya wakulima. Mfano halisi
huko Mtwara wakulima wamekuwa wakilalamikia kuibiwa maelfu ya korosho
wanapopeleka kwenye maghala, sijawahi kusikia hata waziri mkuu au Rais
akizungumzia jambo hilo.
Inakuwaje mtu anaibiwa korosho kwenye ghala,
halafu wakulima hawafidiwi, huu ni wizi wa wazi, ambao hautakiwi
kuvumiliwa,” anasema Ali Msembe, muuza dawa za asili anayezitembeza
Jijini Dar es Salaam aliyeacha kazi ya kufuga eneo la Mdaula, mkoani
Morogoro.
“Asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima, ni
wazi kwamba kama wangesaidiwa, umaskini ungetoweka. Cha kushangaza ni
kawaida kuisikia Serikali ikisema haina fedha...tunashangaa hizo fedha
wanazotumia kwenye mambo mengine kama mchakato wa katiba, kulipana
bungeni, zilizoibwa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) wanazitoa
wapi...tatizo kubwa ninaloliona nchini ni kwamba Serikali haina nia
thabiti ya kuwasaidia wakulima,” anasema Msembe, baba wa watoto wanne
mkazi wa Morogoro.
Taarifa za vyombo vya habari hivi karibuni zinaeleza wakulima Mtwara wamekuwa wakipeleka korosho kwenye maghala kwa ajili ya kuuzwa, huko baadhi huibwa, halafu wanaoiba hawachukuliwi hatua. Kwamba hata viongozi wa Serikali wamekuwa kimya.

Hivi karibuni kulifanyika mkutano wa viongozi wa
nchi za Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia, walisema ni wakati kwa bara
la Afrika kuwa na kilimo chenye tija na kujitosheleza kwa chakula.
Kamishna wa Kilimo na Uchumi wa
Mashambani kutoka Tume ya Umoja wa Afrika, Peace
Tumusiime anasema uzalishaji wa chakula umebaki kuwa chini kwa sababu
bado watu binafsi hawajawekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya kilimo
katika bara hilo. Anasema kinachohitajika ni kwa Serikali kuangalia
namna ya kushawishi na kushirikiana na sekta binafsi kwa vitendo
kuboresha kilimo.
Tumusiime anasema mbali na kushindwa kuwekeza, pia
teknolojia ya kilimo iko chini. Hali hii imekuwa ikisababisha watu
wanaojihusisha na kilimo kuendelea kupungua, hata waliosalia wengi ni
wazee huku vijana walio wengi wakihamia mijini na kukimbia vijijini.
Mkurungezi wa Tume ya Kiuchumi ya Afrika, Carlos
Lopes anasema licha ya Afrika kuwa na rasilimali nyingi za kiasili bado
limekuwa ni bara lenye upungufu mkubwa wa mazao yakiwamo ya biashara na
chakula duniani, sababu kubwa ni usimamizi usiothabiti wa rasilimali
hizo.
“Licha ya bara la Afrika kuwa na rasilimali nyingi
za kiasili bado linasalia kuwa bara lililo na upungufu mkubwa wa
chakula duniani”anasema Lopes.
Katika mkutano huu, viongozi hao walijadili njia
bora za kuimarisha kilimo, kushirikisha wanawake kwenye sekta hiyo na
kuunda sera za kuongoza uzalishaji mzuri wa mazao.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Intertechnology
Ltd, inayouza matrekta Dk Francis Mayaka anasema matrekta yakitumiwa
vizuri yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha kilimo nchini.
“Sera ya Kilimo Kwanza inapaswa kwenda pamoja na uendelezaji na
uboreshaji wa miundombinu kama barabara zinazosaidia usafirishaji wa
mazao”anasema.
Anthony Kerenge ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka
Kampuni hiyo anasema lengo la kampuni hiyo ni kutoa fursa kwa wakulima
wadogo na wakubwa kuinua kununua matrekta kwa gharama nafuu. Anasema
wapo katika hatua za mwisho za majadiliano kati ya Benki ya TIB na Amana
ili kuangalia namna wakulima wanaweza kukopeshwa na hatimaye kulipa
mkopo huo ndani ya miaka miwili.
“Hatua hii ni moja kati ya mikakati tuliyojiwekea
katika kuunga mkono Sera ya taifa ya Kilimo Kwanza ambayo ni mhimili
mkubwa katika kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo mwaka 2025,” anasema
Kerenge.
Karenge anasema kuwepo kwa trekta ya bei nafuu
nchini kutaipunguzia Serikali hasara ambayo ingeipata katika kuagiza
matreka kutoka nje ya nchini na kwamba kampuni yake inaleta matrekta
hayo ili kusaidia wananchi kununua au kukopa kwa gharama nafuu na hivyo
kukuza uchumi.
“Tumeshaanza kutembelea wananchi wa vijiji
mbalimbali na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuwekeza katika Kilimo kwa
kutumia matrekta”anasema Karenge.
Mmoja wa wakulima ambao wametembelewa ni kutoka
Wilaya ya Hannang, Mursal Ayub anasema wakulima wengi wanashindwa
kufikia malengo yao ya kujiimarisha kwa kukosa dhana bora za kilimo.
“Mkulima anapokuwa na dhana bora za kilimo anakuwa
na uhakika wa kufikia malengo yake kuliko yule ambaye hana zana bora za
kilimo, kilimo chake kitakuwa cha kusuasua, hivyo basi ni bora kila
mkulima akawekeze fedha zake katika kununua dhana bora za
kilimo,”anasema Ayub.
Jumla ya matrekta yaliyopo:
Msemaji wa Wizara ya Kilimo na Chakula na
Ushirika, Richard Kasuga anasema hadi sasa kuna Matrekta makubwa 9148 na
madogo 5520 yanayofanya kazi nchi nzima.
Ongezeko hilo limepunguza utegemezi wa jembe la
mkono kwa wakulima nchini kutoka asilimia 70 mwaka 2008 hadi kufikia
asilimia 62 mwaka 2013.
Mikakati ya Serikali:
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Pembejeo na Zana za Kilimo nchini, Mariam Nkumbi anasema wanajipanga
kutoa mikopo zaidi kwa wakulima, na kwamba kila mwaka wamekuwa wakitoa
ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mazao ya mpunga, mahindi, mtama,
alizeti pamoja na miche bora ya zao la chai na kahawa.
“Sasa tupo katika maandalizi ya kutoa mikopo”anasema Nkumbi na
kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya dawa kwa ajili ya mazao
ya Pamba na Korosho na hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa uzalishaji
wa chakula nchini kutoka tani 13milioni kwa mwaka 2012/2013
ikilinganishwa na mahitaji ya tani 11.9milioni yaliyohitajika, sawa na
asilimia 113.
Vile vile msimu wa kilimo 2013/2014 Serikali
ilutumia Sh112.5 bilioni sawa na asilimia 20 ya bajeti ya ruzuku kutoa
mikopo kwa vikundi vya wakulima katika mikoa saba nchini ambayo ni
Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Manyara, Geita na Shinyanga.
Jumla Sh112 bilioni zimetumika kugharamia ruzuku
ya pembejeo kwa msimu wa kilimo 2013/2014. Kwa mwaka 2013/14 Serikali
imetumia Sh 69bilioni kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na Sh15 bilioni kwa
ajili ya ruzuku ya mbegu bora huku ruzuku ya dawa kwa mazao ya Pamba na
Korosho ikiwa ni Sh 3.5 bilioni.
Waziri Chiza:
Waziri wa Chakula, Ushirika na Kilimo, Christopher
Chiza anasema kuanzia msimu wa kilimo 2013/14 hifadhi ya taifa ya
chakula (NFRA) ilikuwa na akiba ya nafaka tani 25,453 na kwamba ilinunua
tani 219,377 na kuwa na jumla ya tani 244,830.
Chiza anasema Serikali imekuwa ikitoa ruzuku za
pembejeo za mbegu bora kwa wakulima kwa utaratibu wa vocha, mwaka
2008/09 ilitoa kwa kaya 737,000, mwaka 2009/2010 kaya 1.5milioni, mwaka
2010/2011 kaya 2.1milioni.
Anasema pia, mwaka 2011/2012 kaya 1.7milioni,
mwaka 2012/2013 kaya 940783, huku mwaka 2013/2014 wizara ilitoa ruzuku
ya pembejeo za kilimo kwa kaya 932,100 ambazo zilitumia tani 124,685 za
mbolea na tani 9621 za mbegu na kati ya hizo , jumla ya tani 36.7 za
mbole zilikuwa chini ya kiwango na hatua za kisheria zilichukuliwa dhidi
wa wahusika.
Hata hivyo licha ya kutoa ruzuku hiyo, pia
uzalishaji wa mahindi uliongezeka kutoka magunia matano hadi kufikia
magunia 15 kwa ekari moja na zao la mpunga limeongezeka kutoka gunia nne
hadi kufikia gunia 20 kwa hekari moja.
Bado Tanzania haijatekeleza maazimio ya Maputo ya
mwaka 2003 ambayo yanazitaka nchi wanachama kutenga asilimia 10 ya
bajeti ya jumla katika matumizi ya chakula na kilimo pamoja na
kuzingatia mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 kwa bajeti ya Matumizi ya
kawaida na shughuli za Maendeleo.
Hata hivyo baadhi ya wakulima wanalalamika kuwa
inachosaidia Serikali kwa wakulima ni kidogo mno, huku wengine wakisema
hakuna usawa katika msaada huo.
“Kuna mikoa haisaidiwi vizuri ukilinganisha na
mingine.Lakini zaidi ni kwamba hakuna harakati thabiti za kuimarisha
kilimo...kuwe na kampeni za kuimarisha kilimo kama tunavyofanya kampeni
za kutokomeza Ukimwi nk,” anashauri James Hangana, mkulima anayefanya
kazi ya kuuza mitumba Kariakoo Jijini Dar es Salaam baada ya kuachana na
kilimo toka Arusha.
Wakulima wengi wanaamini kwamba kama Serikali
ingeongeza nguvu katika kusaidia wakulima, Tanzania ingekuwa na
maendeleo makubwa sana kutokana na ukweli kuwa maeneo mengi nchini yana
rutuba nzuri kwa kilimo.

Chapisha Maoni