HOME
Wanaharakati wa usawa kijinsia nchini wamesema hatua
ya rasimu inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba (BMK) kuacha
baadhi ya madai yao, haijawateteresha, bali imewaingiza kwenye awamu ya
pili ya mapambano kuhakikisha yanaingizwa kwenye katiba mpya ya nchi.
Wamesema wana kila sababu ya kuisifia na kuitetea rasimu ya katiba iliyopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, kwa kuwa imeingiza madai yao kwa asilimia 90.
Walisema hayo katika kongamano lao lililojadili masuala muhimu kwenye mchakato wa katiba mpya, jijini Dar es Salaam jana.
Mwanaharakati, ambaye ni mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ussu Mallya, alitaja ‘mapengo’ yaliyomo kwenye rasimu inayopendekezwa na BMK, kuwa ni pamoja na mchakato kutokuwa na maridhiano na kutokuwa na makubaliano juu ya aina ya Muungano unaopaswa kuwapo nchini.
Mengine ni haki za msingi za huduma za jamii, kufutwa ukomo wa wabunge, uwezo wa wananchi kuwaondoa wabunge, kuongeza madaraka ya Rais, kutotenganisha wabunge na uwaziri na sifa ya mtu kuwa mbunge.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Profesa Ruth Meena, alisema asilimia 90 ya madai yao, ambayo yalikuwa 12 waliyoyawasilisha kwenye Tume ya Warioba yaliingizwa kwenye rasimu ya kwanza na ya pili ya tume hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mikataba na matamko mbalimbali ya kimataifa na kikanda yaliyoridhiwa na serikali na kusema huo ni ushindi mkubwa kwao.
Baadhi ya madai hayo ni pamoja na kuwapo usawa wa asilimia 50 kwa 50 kwenye vyombo vya maamuzi, kujenga nchi isiyokuwa na ubaguzi wa kijinsia, usawa wa kijinsia kama msingi wa utawala bora, haki sawa za uraia, mgombea huru, mwanamke kurithi ardhi na vyama vya siasa kuzingatia uwakilishi sawa.
Wanaharakati kutetea Rasimu ya Warioba
Mwanaharakati, ambaye ni mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ussu Mallya

Chapisha Maoni