Raila Odinga alichapwa mara mbili kwa kiboko katika tukio ambalo limewashangaza wengi
Hali
ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale
nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza
kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa
wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa
wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa
jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa
wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan
Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Mwanamume huyo alimshambulia
Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya
kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo
mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani
kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni
kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke
aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake
waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.