HOME
DODOMA
DODOMA
Bunge la
11 limeendelea tena leo April 22 2016, Waziri mkuu Kassim Majaliwa
amehutubia bunge kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na
makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu kwa
mwaka 2016/2017.
Katika kitengo cha huduma ya Jamii Elimu, Waziri Majaliwa amesema ‘Kwa
kutambua umuhimu wa Elimu kama nyenzo imara ya maendeleo ya kiuchumi na
kijamii, Serikali imeanza kuboresha na kuimarisha elimu ya awali,
msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.’
‘Baada
ya kuanza utekelezaji wa mpango wa elimu bila malipo, kumejitokeza
changamoto kadhaa, ikiwemo miundombinu kama madarasa, mabweni, maabara,
nyumba za walimu na vyoo‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na jitihada kubwa zimewekwa‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘Nitumie
nafasi hii kuwashukuru wadau walioanza kuchangia madawati katika maeneo
mbalimbali,na niwasihi wengine waendelee kuunga mkono Serikali yao‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘Kuanzia
leo hii, nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliokamata mbao
ndani ya Halmashauri zao kuzitumia kutengeneza madawati na siyo
kuzipiga mnada‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘Hali
ya urejeshaji wa mikopo iliyotolewa hairidhishi, Hivyo naagiza Bodi ya
mikopo ya Elimu ya Juu kufuatilia urejeshaji wa mikopo hiyo ili fedha
hizo zitumike kuwakopesha wanafunzi wengine;
Chapisha Maoni