Unknown Unknown Author
Title: FISI AJERUHI WATATU GEITA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Thursday19/06/2014         FISI AJERUHI WATU WATATU HUKO GEITA, MMOJA ALIWA MDOMO MENO YABAKI WAZI WATU watatu waliot...

Thursday19/06/2014


       

FISI AJERUHI WATU WATATU HUKO GEITA, MMOJA ALIWA MDOMO MENO YABAKI WAZI


WATU watatu waliotambulika kwa majina Bugema Nzombe (21) Peter Francis (32) Manoni (23) wakazi wa mjini katoro wilayani Geita mkoani hapa wamejeruhiwa baada ya kung”atwa na Fisi sehemu mbalimbali za miili yao .


Ofisa mtendaji wa kata ya Katoro Aloys Kamuli alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi Majira ya saa 7.45 mchana katika eneo la kisima cha Kabahelele kitongoji cha Bulenganhansi Katoro baada ya fisi huyo ambaye alikuwa akikimbizwa na wananchi akitokea eneo la Mnadani Katoro kufika katika eneo hilo na kisha kuanza kuwa kimbiza wachotomaji waliokuwa eneo hilo .


Ameogeza kuwa katika tukio hilo watu watatu wamejeruhiwa ambapo Manoni amejeruhiwa vibaya sehemu usoni na amenyofolewa mdomo wa juu na meno yake kubaki wazi na fisi huyo na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi na wengine kupelekwa katika kituo cha Afya Katoro .


Aidha alisema kuwa tukio liliibua hofu kubwa kwa wananchi wa eneo hilo lakini baadae hali ya amani ilirejea baada ya fisi huyo kuzingirwa na wananchi na kisha kuingia kwenye nyumba moja na ndipo na wananchi waliamua kufunga mlango wa nyumba hiyo kwa nje na kuomba msaada kwa askari wa kituo cha polisi ambapo askari watatu wakiwa na askari mgambo mmoja akiwa na silaha (Bunduki) walifika eneo hilo na kufanikiwa kumuua fisi huyo .


Mganga wazamu katika kituo cha Afya katoro Dk Daniel Izengo amekiri kuwapokea majeruhi wawili jana majira ya saa 8.40 mchana na kusema kuwa Peter amenyofolewa vidole viwili vya mkono wa kushoto pia amejeruhiwa paja la mguu wa kushoto na fisi huyo na Bugema amejeruhiwa mguu wa kulia
.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wameli husisha na tukio hilo na imani za kishirikina fisi hawezi kuishi karibu na makazi ya watu na kusema kuwa hili ni tukio la kwanza kutokea tangu kata hili ya asili kuanza kati ya mwaka 1978.


Na Valence Robert- Geita
        

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top