Thursday, June 19, 2014
SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SHISHA
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti
ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi
sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana wadogo mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na tisho
la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavitaji wa sigara.
Chapisha Maoni