NGURUWE MBARONI UGANDA KWA "UGAIDI"
Polisi nchini Uganda wanawafanyia uchunguzi nguruwe wawili kuhusiana na "ugaidi" baada ya wanyama hao kuingia katika eneo la bunge.
Taarifa zinasema nguruwe hao watoto walikuwa wamepakwa rangi za chama tawala na kubebeshwa mabango yanayowatuhumu wabunge kwa ufisadi.
Watu wawili wanaoshukiwa kutekeleza tukio hilo wanashikiliwa na polisi wakisubiri kuburuzwa mahakamani mjini Kampala.
Askari polisi kadhaa wamesimamishwa kazi kufuatia tukio hilo na wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazi, amekaririwa msemaji Polly Namaye na shirika la habari la AFP.
Msemaji huyo amesema nguruwe hao wanafanyiwa uchunguzi wa "kigaidi" kama ulivyo utaratibu.

Chapisha Maoni