Jumanne24/06/2024
SEKRETARIETI YA AJIRA YA ZIPA RUNGU SERIKALI ZA MITAA
Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Akihojiwa
katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi
wa Umma, Riziki Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo
itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wa jira
serikalini kwa serikali za mitaa.
“Sekretarieti
ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha
mchakato wa ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation
staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka
wa fedha 2014/15” alisema.
Pia,
alisema katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa waombaji,
Sekretarieti hiyo haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ).
Alieleza kuwa zipo kada, ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo kada ambazo
kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa zilizoainishwa.
“Zipo
baadhi ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwango
fulani. Kada ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za
wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine hazina masharti ya GPA,
kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa katika tangazo la
nafasi za kazi kulingana na kada husika”, alisema Riziki.
Alitaja
moja ya matatizo wanayopata waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na
vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa kazi ambao wamepata tatizo
hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye mamlaka husika, alikokuwa
amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na kutangaza
kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari (gazeti).
“Ikithibitika
hivyo mamlaka husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa
kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu
waliopoteza vyeti na hatimaye huruhusiwa kufanya usaili” alisema.
Chapisha Maoni