Unknown Unknown Author
Title: KIKWETE ATAMANI UKUNZI JKT
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jumapili 22/06/2014      KWA HABARI ZA NYUMBANI TANZANIA...... RAIS KIKWETE ATOA MHADHARA KATIKA CHUO CHA ULINZI JIJINI DAR ES SALAAM...
Jumapili 22/06/2014


    
KWA HABARI ZA NYUMBANI TANZANIA......
RAIS KIKWETE ATOA MHADHARA KATIKA CHUO CHA ULINZI JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa mhadhara kuhusu Fursa (A lecture of Opportunity) katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo
Pia Rais Kikwete amesema kuwa hana wasiwasi na hali ya mjadala mkali uliotawala Bunge Maalum la Katiba kwa sababu ni muhimu kwa mjadala kuhusu Katiba Mpya ukawa wa kina ili kuweza kupata Katiba bora kwa Watanzania.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Katiba ya Tanzania haitapatikana kwa mikutano ya kisiasa nje ya Bunge Maalum la Katiba bali ndani ya Bunge hilo ambako ni dhahiri kuwa mjadala utatawaliwa na nguvu ya hoja na busara.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ametoa ufafanuzi wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa Taifa (The Security of the Nation) kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi – National Defence College – kilichoko Kunduchi, Dar Es salaam.
Wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ofisa mmoja wa Jeshi la Kenya alimwuuliza Rais Kikwete kama alikuwa na wasiwasi kuhusu mjadala unaoendelea nchini kuhusu Katiba Mpya unaweza kuvuruga usalama wa Tanzania.
Rais Kikwete amemjibu: “Sina wasiwasi hata kidogo kwa sababu hatukutarajia kuwa mjadala wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu jambo hili kubwa ungekuwa rahisi. Yalipojitokeza maoni ya Tanzania kupata Katiba Mpya, tuliunda Tume na tume hiyo ikatoa ripoti yake ambayo ndiyo inajadiliwa katika Bunge Maalum. Hatukutarajia kuwa mjadala kuhusu ripoti ungekuwa rahisi kwa wajumbe kutoa majibu ya ndiyo ama hapana.”

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top