Jumamosi21/06/2014
WATU SITA WAPOTEZA MAISHA ENEO LA MAKONGO
Watu
zaidi ya 6 wamepoteza maisha papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa vibaya
kwenye ajali ya Daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo - Tegeta
jijini Dar mchana huu,baada ya kushindwa maarifa ya kiudereva kwa
Dereva wa daladala hilo hali iliyompelekea dereva huyo kuhama mpaka
upande wa pili wa barabara na kulivaa lori kwa nyuma.Chanzo cha ajali
hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.
Ajali hiyo inadaiwa kuhusisha magari manne yaliyo gongana huku Daladala hilo ndilo likiwa limep[ata madhara makubwa.
Ajali hiyo inadaiwa kuhusisha magari manne yaliyo gongana huku Daladala hilo ndilo likiwa limep[ata madhara makubwa.

Hili ndilo lori lililokuwa likipita katika upande huo wa Barabara na kufatwa na daladala hiyo.

Chapisha Maoni