Vurugu kubwa
zimetokea katika kijiji cha Buyango wilayani Muleba mkoani Kagera baada
ya wazazi kuikataa maiti ya mtoto wao kwa madai amenyofolewa viungo
vyake vya mwili hali iliyosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi
kutawanya makundi yaliyofunga barabara na kubomoa chumba cha kuhifadhia
maiti kutafuta viungo hivyo.
Vurugu hizo
zimetokea baada ya mama mmoja mkazi wa Arusha aliyepeleka maiti ya
mtumishi wake wa ndani na kuwakabidhi wazazi wake kwa masharti ya
kutoifunua hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa ambapo mama huyo
amelazimika kwenda hospitali kukabidhi mwili huo ambapo baadhi ya ndugu
na jamaa walivamia chumba cha kuhifadhi maiti na kubomoa mlango kisha
waka angalia mwili ambao wameukuta ukiwa na majeraha na kwamba haufanani
na binti yao aliyefahamika kwa jina la Ajela Tilifon mwenye umri wa
miaka 16 aliyechukuliwa kijijini hapo tangu mwaka 2012 kwa lengo la
kwenda kufanya kazi za ndani mjini Arusha na kwamba baada ya ndugu
kukataa kupokea mwili askari polisi wamewakamata ndugu na mwaandishi wa
habari kwa madai kuwa wanahamasisha vurugu.
Kufatia hali
hiyo mkuu wa wilaya ya Muleba Bw. Lebris Kipuyo alilazimika kufika eneo
la vurugu na kuamuru askari polisi kutawanya wananchi ili magari yaweze
kupita na baadaye alifika hospitali na kuteuwa baadhi ya ndugu,jamaa na
wazazi wa mtoto ambao walikagua mwili wa marehem kisha mkuu wa wilaya
akawahutubia wananchi na kuwataka walioshuhudia mwili waseme ukweli
walichokiona nao bila kusita wamesema maiti inamajeraha tumbo
limetobolewa na sehemu za mwili zimekwaruzika kisha akavishwa nguo na
soksi ili kuficha ukweli.
Naye mwaandishi
wa habari wa kujitegemea gazeti la Mwananchi aliyejeruhiwa na askari
polisi kwa kupigwa virungu Bw. Shaban Ndyamkama amesema kuwa yeye ndiye
aliyetoa taarifa za vurugu hizo kwa mkuu wa wilaya ya Muleba baada ya
askari kufika eneo la tukio walimkamata na kumshambulia kwa vipigo kisha
wakamshikilia kwa muda hadi wananchi waliposhinikiza kuachiwa kwake na
baada ya waandishi wa ITV,Radio one kanda ya ziwa kumuomba kamanda wa
polisi mkoa wa Kagera Bw. George Mayunga ambaye amekiri kwa njia ya simu
kuwa vurugu hizo zimesababisha uvunjifu wa amani na kumtaka mkuu wa
polisi wilaya ya Muleba kumuachia huru mwaandishi wa habari ambaye
amepelekwa hospitali na wananchi kwa matibabu zaidi
Chapisha Maoni