Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Boss wa TBS aliyehukumiwa kwenda jela miaka mitatu. Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam August 28 2014 imetoa hukumu k...
HOME

Boss wa TBS aliyehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.

Screen Shot 2014-08-29 at 8.32.31 AMMahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam August 28 2014 imetoa hukumu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekerege kifungo cha miaka 3 jela.
Ripota wa malundelubuyi.com amesema Charles alifikishwa kizimbani akikabiliwa na makosa mawili likiwemo moja la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya dola za kimarekani 42,543 ambapo kesi hiyo ilifunguliwa Novemba 06 2013.
Screen Shot 2014-08-29 at 8.38.50 AMMshitakiwa alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni; (1) Matumizi Mabaya ya Madaraka kinyume na kifungu cha sheria F 31 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 na (2) kusababisha Hasara ya kiasi cha USD 42,543/= sawa na Tsh. 68,068,800/= kwa Shirika la Viwango Tanzania – TBS.
Ni kinyume na kanuni za adhabu – K/A 10(1) ya jedwali la kwanza ikisomwa pamoja na vifungu 57(1) na 60(2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 kwa kusitisha ulipwaji wa 50% ya ada ya Utawala (Administrative fee) kwa kampuni za JAFFAR MOHAMED ALI GARAGE and QUALITY MOTO pamoja na kosa jingine ambalo ni matumizi mabaya ya madaraka.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top