HOME
HALMASHAURI YA MSALALA YAPIGWA MARUFUKU KUFANYA SHEREHE WALA MIKUTANO.
Serikali wilayani Kahama kupitia kamati yake ya Ulinzi
na Usalama ya wilaya imepiga marufuku kufanyika kwa mikutano,maandamano pamoja
na sherehe kwa wananchi wote wa Halmashauri mpya ya Msalala baada ya kubaini
kuwepo kwa uvunjaji wa amani.
Hali hiyo imetangazwa jana
na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama
ya wilaya ya Kahama Benson Mpesya baada ya kubaini kuwepo kwa
mikutano,maandamano pamoja na sherehe baada ya Waziri Mkuu;Mizengo Pinda
kutangaza Makao Makuu ya Halmashauri hiyo Busangi.
Wananchi hao kupitia madiwani
wao walikuwa na Mgogoro wa siku nyingi wa kugombea Makao Makuu hayo,ambapo
awali wakati wa kuanzishwa kwa halmashauri hiyo ya Msalala,serikali ilitangaza makao makuu hayo
kuwa kata ya Busangi.
Hata hivyo baada ya muda baadhi
ya Madiwani walibadirisha Makao Makuu hayo kwa kuyahamishia Kata ya Segese hali
ambayo ilizua mvutano mkubwa wa kugombea ujenzi huo hali ambayo Waziri Mkuu aliingilia
kati kupinga kuhamishwa kwa Makao hayo.
Kufuatia hali hiyo mwishoni
mwa wiki iliyopita wananchi wa Msalala waligawanyika kwenye makundi mawili
ambapo wengine waliunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu kwa sherehe huku wengine wakipinga kwa maandamano na mikutano.
Hali hiyo kwa mujibu wa
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkuu ya wilaya ya Kahama amesema ili kulinda
amani kwa wananchi Serikali imepiga marufuku mikutano ama mikusanyiko ya aina
yoyote mpaka pale watakapotangaziwa.
Chapisha Maoni