HOME
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Jaji Mstaafu Joseph Warioba licha ya kushambuliwa na mambo ya msingi anayozungumza kuhusu Katiba mpya hakuna mtu aliyejitokeza kujimbu hoja zaidi ya kumpiga vita kwa kutumia njia wanazozijua.
Warioba alisema watu hao wanaomshambulia wamekua wakitoa majibu mepesi kwamba yeye anamsaliti Mwalimu Nyerere lakini kwa mambo anayoyazungumza hata Mwalimu akija leo atamuunga mkono.
Alisema kama tunataka kupata kitu kizuri hatuwezi kukipata kwa kutumia lugha za matusi wala kejeli.
“Mimi nimekua nikizungumza mambo ya msingi kuhusu Katiba iliyopendekezwa lakini hakuna anayejitokeza na kunijibu zaidi ya kunijibu kwa mambo mengine wanayoyajua wao”alisema Warioba.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi MkoaniSingida linamshikilia Nawaridi Saidi mwenye miaka 45 mkazi wa Dar es salaam kwa tuhuma za kumtupa mjukuu wake Mayasa Meshack mwenye miaka sita kutoka ndani ya basi wakati akisafirikwenda Kigoma akitokea Jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi Thobiasi Sedoyeka alisema tukio hilo lilitokea Desemba 18 saa 2 usiku Wilayani Iramba ambapo mama huyo akiwa kwenye basi aina ya Scania alifungua dirisha kutoka kwenye kitialichokaa na kumtupa Mayasa wakati basi likiwa kwenye mwendo kasi.
“Mama alikua anaenda Mkoani Kigoma kwa ajili ya sikukuu za Krismas na mwaka mpya aliambatana na mtoto wake mwingine ambaye jina halikutambulika,na baada ya kumtupa mtoto huyo abiria wengine walipiga kelele zilizomuamuru dereva asimamishe gari na kurudi nyuma kumwokota mtoto huyo ambaye bado alikua hai”alisema.
Baada ya kuokotwa alikimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida na kuanza kutibiwa haraka lakin ba ada ya muda mtoto huyo alifariki dunia.
Katika maelezo hayo mama huyo alisema anatatizo na kuumwa kichwa na kupoteza kumbukumbu mara kwa mara ,hivyo hakumbuki kama alitenda kosa hilo lakini alishtuka baada ya kupigwa na abiria waliokuwemo ndani ya basi.
MTANZANIA
Sasa kuna kila dalili ya Serikali kuingia katika kashfa nyingine mpya ya Sukari baada ya ile ya uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 ya akaunti ya Tegeta Escrow kutikisa nchi.
Dalili hizo zimeanza kujitokeza sasa wakati uchunguzi umebaini kufurika wa sukari katika soko,msingi wake ni mkakati wa kufadhili mbio za uchaguzi mkuu wa Urais mwakani.
Imebainika kuwepo na wafanyabiashara wanaoagiza sukari kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na nyingine kwa matumizi ya viwandani lakini wanaiuza nchini kwa ajili hailipiwi kodi huku wakidai kufadhili makundi ya wagombea urais.
Katika mkakati huo uliozaa kashfa iliyopewa jina la ‘Whitegold Scandal’ yanatajwa baadhi ya majina ya wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na biashara hiyo ambao wamekua wakikingiwa kifua na vigogo waliokondanina nje ya serikali kwa kuwapa vibali vya kuagiza bidhaa hiyo nchini pasipo kukatwa kodi.
MTANZANIA
Kwa mara ya pili jina la Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa limetajwa kwenye ripoti ya kitengo cha utafiti cha jarida la Economist Intelligence Unit EIU kuwa ndiye mwanasiasa anayekubalika zaidi ndani ya CCM kuwania Urais mwakani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya EIU yenye makao yake makuu London,Uningereza ilitolewa December 19 mwaka huu na ushindani unaoendelea kwa sasa baina ya wanasiasa sita wanaodaiwa kuendesha kampeni za kuwania urais mwakani utakigawa Chama hicho,lakini hautakinyima ushindi.
Makada wa CCM wanaodaiwa kuwania kiti cha Jakaya Kikwete ni pamoja na Lowassa,Waziri mkuu Pinda,Fredrick Sumaye,Willium Ngeleja,Bernad Membe,Steven Wassira na January Makamba.
Ukimuacha Pinda makada waliosalia katika orodha hii wamekwishatiwa hatiani na kamati kuu ya CCM kwa kuendesha kampeni za kuwnaia nafasi hiyo kinyume na sheria jambo ambalo limezua mgawanyiko wa kimakundi na kuhatarisha umoja ndani ya Chama hicho.
“CCM itagawanyika katika kumpata mshindi wa kiti cha urais,nakundi la Waziri mkuu wa zamani Lowassa ndilo linaloonekana kuwa na nguvu kubwa ya mgombea wake kuteuliwa kuwania Urais,,,hata hivyo Pinda anafanya vizuri na sasa kundi lake ndilo linaloshika nafasi ya pili nyuma ya lile la Lowassa”lilieleza jarida hilo.
JAMBOLEO
Hospitali ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita ina tatizo kubwa na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti hali inayosababisha zihifadhiwe kwenye korido.
Hali hiyo ilibainika baada ya mwalimu wa shule ya Msingi Kasandalala Wilayani humoLaideth Constantine mwenye miaka 33 kuthibitika kuwa alimnyonga mtoto wa miaka saba na maiti yake kuhifadhiwa kwenye korido.
Kutokana na tukio hilo Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Cosmas Kilosa alisema hospitali hiyo ina changamoto kubwa ya kukosa sehemu ya kutunza maiti hali iliyosababisha maiti hiyo kuhifadhiwa kwenye korido.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo alisema mwalimu huyo anashikiliwa na Polisi baada ya vipimo vya daktari kuthibitisha kuwa mtoto huyo kanyongwa.
Alisema mwili wa marehemu ulikua umejaa damu nyeusi,uvimbe pamoja na kutokwa na ulimi mrefu nje na inasemekana mwalimu huyo ndiye aliyehusika na tukio hilo.
Hizi ni zile Stori zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 21, 2014

Chapisha Maoni