HOME
Nilikurekodia sauti na Video wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha K24, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.
Kutoka Kenya, maiti imezikwa baada ya mgogoro wa familia uliodumu kwa miaka mitano
Katika
hali ya kushangaza familia moja ilijikuta katika hali ya furaha kwenye
msiba, wakaimba na kucheza ngoma tofauti na ambavyo tumezoea kwamba
msibani ni sehemu ambayo watu huwa na majonzi na huzuni.
Furaha hiyo ilitokana na kitendo cha
Mahakama kuruhusu mazishi ya ndugu wa familia hiyo huko Kenya baada ya
mwili wa marehemu huyo kukaa zaidi ya miaka mitano ndani ya chumba cha
kuhifadhia maiti kutokana na kesi ya mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya
marehemu na ndugu yake.
Ardhi ambayo ilikuwa ikigombaniwa ni
sehemu ambapo alipaswa kuzikwa marehemu huyo, hivyo kutokana na kesi
hiyo wakashindwa kufanya mazishi, wiki hii Mahakama kuu ya Nyeri
iliruhusu mwili huo kuzikwa eneo hilo ambalo lilikuwa na mgogoro wa muda
mrefu.
Kutoka kwenye taarifa iliyoripotiwa na Kituo cha K24, mwanakijiji mmoja alisema; “…
sisi tulipanga mazishi, huyu kijana hakuweza kuzikwa kwa sababu huyu
Mzee alienda kortini na kuweka ile mnaita ‘Court Injunction’ kwamba
hawezi kuzikwa katika hili shamba, kwasababu iko na kesi na shamba ni
yake kwa hiyo mtu hawezi kuzikwa katika hiyo shamba yake, hiyo ndiyo
kesi imekuwa ikiendelea...”
Nilikurekodia sauti na Video wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha K24, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.
Chapisha Maoni