HOME
Mama amekaa kando akifurahia moto unavyowaka, familia yateketea ndani ya nyumba
Polisi
nchini Japan imemfungulia mashtaka mwanamke mmoja baada ya kuona moto
ukiunguza nyumba yake huku akishuhudia na kushindwa kutoa taarifa kwa
jeshi la Zimamoto pamoja na watu waliokuwemo ndani.
Sababu za mwanamke huyo mwenye miaka 36
kuamua kukaa kimya alijitetea kuwa alikua akipenda kuona jinsi moto huo
ulivyokua ukiwaka na hakujali thamani ya vitu vyake vilivyokua ndani ya
nyumba hiyo.
Mwanamke huyo alikua akiishi floo ya
kwanza ya jengo hilo katika mji wa Kagoshima pamoja na watoto wake
wawili wa kike pamoja na mama yake mzazi.
Aliripotiwa kuwa licha ya kuuona moto
huo hakufanya lolote na kuanza kuushangaa ulivyokua unasambaa ndani ya
nyumba hiyo mpaka watoto wake waliposikia harufu ya moto wakiwa wamelala
na kukimbia kwenda kumwamsha bibi yao mwenye miaka 70,lakini jitihada
zao hazikufanikiwa baada ya bibi huyo kuchelewa kuamka na wao kuamua
kukimbia nje na kumwacha akiteketea.
Polisi waliamua mshtaki mwanamke huyo
kwa kosa la kukusuadia lakini alikiri amekosea lakini alisema alikua
anapenda kuona moto ulivyokua ukiwaka.
Chapisha Maoni