HOME
MWANANCHI
Mkazi wa Wilaya ya Kilombero,Morogoro Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo.
Ofisa Mtendaji wa kata ya Mang’ula Shabaan Lichaula na Mkuu wa kituo cha Polisi Nkilijia Lazaro walisema Polisi inamshikilia mwanamke huyo ambaye ni mke wa marehemu wakati wakimsaka mtuhumiwa.
Lichaula alidai marehemu katika kumtafuta mkewe alimkuta amesimama mahali na mwanaume huyo na baadaye mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu kuamua kumvaa mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni hadi utumbo kutoka nje.
Alisema baada ya marehemu kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema walijitokeza na kumwahisha hospitali na alifariki dunia baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza wakati akihamishiwa katika hospitali Mtakatifu Fransis,Ifakara kwa matibabu zaidi.
MWANANCHI
Washtakiwa 11 wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekua mjumbe wa tume ya mabadiliko ya Katiba,Dk Sengondo Mvungi jana waligoma kwa muda kuondoka kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakishinikizwa kuelezwa lilipo jalada la kesi yao na hatua ilipofia.
Hilo lilitokea jana saa nne asubuhi ,muda mfupi baada ya wakili wa serikali,Peter Njikekumweleza Hakimu Hellen Liwa kuwa kesi hiyo ilifika mbele yake kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine.
Mshtakiwa Masunga Makenza alidai hafahamu sheria ,kesi hiyo ni ya muda mrefu na akahoji jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda gani.
Makenza alidai kuwa kesi hiyo ni ya kubambikiwa na kwamba ingekuwa halisi,upande wa mashtaka ungekuwa umekwishakamilisha upelelezi na kwamba wapotayari kushtakiwa ila kama upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie huru na ikikamilisha iwakamate tena.
MWANANCHI
Ikiwa imebaki takribani miezi 1o kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwakani,Chama cha CCM kinaonekana kuteswa na tuhuma za rushwa inayodaiwa kutolewa na makada wake wanaotajwa kutaka kuwania nafasi mbalimbali ukiwemo urais.
Hali hiyo inabainishwa nabaadhi ya makada wa Chama hicho katika ngazi mbalimbali ambao wameamua kulalamika waziwazi kupitia vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
Moja ya kauli ni iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini Khamis Kagasheki kwenye akaunti yake ya Twitter akisema “Mgawo wa Xmass na mwaka mpya kwa wajumbe wa husika wa CCM ni kucheza na ugumu wa maisha uliopo,ni ununuzi wa nafasi na si uwezo wa ongozi, aibu”.
Alipotakiwa kufafanua Kagasheki alisema hakumtaja mtu licha ya kwamba wapo wengi wanaotoa zawadi,lakini baada ya kuandika kwenye mtandao ameandamwa na baadhi ya watu huku wengine wakimtolea lugha chafu.
“Hii ni line yangu naitumia kutoa mawazo siku zote,lakini nashangaa leo watu wameshikia kidedea maoni hayo mpaka wengine wanatumia lugha kali..sijamtaja mtu kwa sababu najua wapo wengi wanaotoa zawadi”alisema.
HABARILEO
Msichana mmoja mkazi wa mtaa wa Zaire Mkoani Arusha,amelazwa katika hospitali ya Mount Meru Arusha chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kujizalisha mwenyewe kisha kumtumbukiza mtoto kwenye ndoo ya maji.
Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikua amepanga chumba cha kuishi,Ruben Mollel alisema msichana huyo alikua anajulikana kwa jina la Dada Pendo na kwamba maisha yake hayakua wazi.
“Alipokuja kupanga hapa alidai yeye ni mwanafunzi,ila hivi karibuni alionekana kuwa mjamzito,hakuna kilichojulikana tena hadi jana ambapo nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto kilichadhaniwa kuwa ni chake kikiwa kimezamishwa kichwa chini kwenye ndoo ya maji”alisema baba huyo mwenye nyumba.
Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto huyo ndani ya nyumba ya dada huyo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake Mama Martha ambaye alidai kuwa alisikia sauti ya mtoto akilia usiku kucha na baadaye kutoweka majira ya asubuhi.
Baada ya juhudi za kuchunguza walikuta kichanga hicho cha kiume kikiwa ndani ya ndoo na tayarikilikua kimefariki dunia huku mama yake akiwa katika hali mbaya kutokana na kujizalisha mwenyewe.
HABARILEO
Mvua iliyonyesha jijini Dar es salam imeleta balaa baada ya kuua watu wawili katika maeneo tofauti ya jiji hilo likiwemo tukio la mtoto wa miaka minne kufa baada ya kuzidiwa na maji yaliyoingia ndani ya nyumba wakati akiwa amelala.
Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Camilius Wambura alisema matukio hayo yalitokea jana mchana kwenye maeneo mawili tofauti.
Tukio la kwanza lilitokea eneo la Tandale ambapo mtoto Nasma Ramadhani akiwa amelala ndani ya nyumba yao maji ya mvua yaliingia ndanina kumzidia nguvu hadi kufariki na mwingine bibi kizee kufariki eneo la Mwananyamala aliyeangukiwa kichwani na ukuta wa nyumba yake na kumsababishia mauti.
Wambura alisema madhara mengine ni maji kujaa kwenye ameneo mbalimbali ikiwemo Mikocheni zilizopo ofisi za Tanesco,Kinondoni jirani na TMJ hivyo kuleta usumbufu wa Magari na watukuvuka eneo hilo.
MTANZANIA
Iliyokua ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa iko katika matengenezo baada ya Wizara ya Maliasili kuridhia itumike kama jengo la Makumbusho ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya hiyo na msaidizi wake wamehamia katika jengo jipya lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 katika eneo la Mawelewele mjini hapa.
Ukarabati wa jengo hilo lililojengwa na Serikali ya Ujerumani zaidi ya miaka 114 iliyopita utafanywa na mradi wa kuendeleza utamaduni Nyanda za juu Kusini.
“Mradi huu wa Utalii ambao ni wa mamilioni ya pesa utahusisha ukarabati na uhifadhi wa iliyokua boma ya Iringa enzi za Utawala wa Kijerumani”alisema Meneja mradi Jan Kuever.
NIPASHE
Shinikizo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo limezidi kushika kasi baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kumuomba Rais Kikwete kumwajibisha ili kupisha nafasi hiyo ili ichukuliwe na mtumishi mwenye sifa ya kutumikia umma.
Kikwete alisema katika hotuba yake kupitia wazee wa Mkoa wa dar es salaam kuwa amemuweka kiporo Muhongo kwa siku mbili hadi tatu kwa kuwa uchunguzi dhidi yake ulikua unaendelea.
Hatahivyo tangu siku hiyo zimeshapita siku tisa bila rais kutangaza hatma ya Muhongo kama anatimuliwa ama anabaki katika nafasi yake.
Jukata wamemuomba Kikwete wamemuomba Kikwete kuchukua hatua dhidi ya Waziri huyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Nimekuwekea hapa Stori muhimu zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya Leo Tanzania December 30, 2014

Chapisha Maoni