HOME
Na Valence Robert0-Malunde1 blog Geita
Ads by SavePass 1.1Ad Options
Jeshi la polisi Mkoani
Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya
waendesha pikipiki (BODABODA), baada ya kuzingira nyumba ya mfanyabiashara
anayesadikiwa kuwa ni mwizi wa pikipiki na kutaka kuichoma moto.
Wakizungumzia
tukio hilo baadhi ya mashuhuda wameimbia Malunde1 blog kuwa mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Juma Joseph (36) mkazi wa
Msalala Road, akiwa amembeba abiria wake Saada Nasorwa (37),
walizingirwa na
waendesha pikipiki wakitaka kuwachoma moto.
Tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi, katika maeneo
ya NMB Bank ambapo watu hao walikuwa wanaendesha pikipiki yao yenye namba T 234
AVH aina ya sanlg kuelekea makao makuu ya polisi Mkoa.
“Sisi tumewaona watu hawa wakipita hapa wakiwa wamebebana
lakini muda mfupi baadaye tuliona waendesha bodaboda wakiwafukuzia huku wakisema ni
wezi, wakamatwe, wachomwe moto, wametuchosha kutuibia pikipiki na kuwaua wenzetu,”walisema
mashuhuda hao.
Inaelezwa kuwa mfanyabiashara huyo Juma amekuwa
akiwatumia vijana kupanga njama mbalimbali
za kuiba pikipiki na wakati mwingine kutekeleza mauaji kwa waendesha bodaboda
jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi wa Mkoa wa Geita.
“Taarifa nyingi za huyu jamaa ziko polisi lakini tunashangaa
kila akikamatwa anaachiwa huru na kurudi uraiani na kutusumbua sisi wananchi kwanini
asifungwe? Na wakati ushahidi tunapeleka yeye ni nani?”alihoji Masanja ambaye
ni mwendesha bodaboda.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amejisalimisha katika
kituo chake ili waendesha pikipiki hao wasimuue na kwamba mali zake zote
zilizokuwa katika soko kuu la Geita zimeharibiwa vibaya na nyingine kuibiwa.
Hata hivyo kamanda Konyo, aliwataka waendesha bodaboda hao
kuwa watulivu wakati jeshi lake likiendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na
kuwataka wananchi wenye taarifa na hilo wazitoe ili mtuhumiwa afikishwe kwenye
vyombo vya sheria.
“Nawaomba waendesha pikipiki wote muwe watulivu wakati
uchunguzi ukiendelea na tunaomba wenye taarifa na hili watupe ushirikiano ili
mtuhumiwa afikishwe mahakamani,”alisema Konyo.
Chapisha Maoni