HOME Purukushani bungeni nchini Kenya wabunge wakiwa katika vikao bungeni...
HOME
Purukushani bungeni nchini Kenya
wabunge wakiwa katika vikao bungeni
Wabunge
wa Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku
wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswada tatanishi wa usalama
ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge
lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili
mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao
maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye
utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwani long'i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo
Mwenyekiti wa kamati ya usalama
wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko
yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na
kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'
Spika
wa bunge Justin Muturi wakati mmoja aliamuru walinzi wa bunge kuwaondoa
baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao
ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo
ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na
mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza
kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Wabunge wakipitisha vipengee vya mswada huo vilivyofanyiwa marekebisho
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia
ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa
faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha
ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa
kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab
wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais
Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui
mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari
la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Chapisha Maoni