HOME
Hatari Geita!! MWENDESHA BODABODA ACHINJWA KAMA KUKU NA MTU ALIYEMKODI PIKIPIKI
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Hatari Geita!! MWENDESHA BODABODA ACHINJWA KAMA KUKU NA MTU ALIYEMKODI PIKIPIKI
Waendessha bodaboda wakiwa katika mkutano wa dhalura kujadili suala la ulinzi na usalama wao -Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita |
Kijana
mmoja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda aitwaye Ismail
Khalid(25)mkazi wa mtaa wa Shilabela kata ya Kalangalala mjini Geita
ambaye ni mwenyeji wa Nyakahula wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera
ameuawa kikatili kwa kunyongwa kisha kuchinjwa akitenganishwa kichwa na
kiwiliwili na mtu aliyekodi usafiri wake wa pikipiki.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 19 mwaka huu saa 5 usiku baada
ya mtu ambaye hakufahamika mara moja kufika eneo la Stand mpya
anapopaki pikipiki yake na kumkodi akimtaka ampeleke katika mtaa wa
Tambukaleli mjini Geita.
Inaelezwa
kuwa mtu huyo alimnyonga na kumchinja shingo kwa kumtenganisha kichwa
na kiwiliwili chake na baadaye kutokomea kizani na pikipiki hiyo.
Kaka
wa marehemu Hassan aliiambia Malunde1 blog kuwa,mwili wa mdogo wake
uligundulika asubuhi ya Desemba 19 mwaka huu mita chache kutoka eneo
alilokuwa akipaki pikipiki yake.
Kwa
mujibu wa majirani kwenye eneo la tukio inavyoonekana wauaji walimuulia
eneo hilo na kutokomea na pikipiki hiyo ambayo hata hivyo namba zake
hazikuwezaa kupatikana mara moja.
Mwenyekiti
wa bodaboda wilaya ya Geita Daniel Dotto mbali na kuthibitisha kuwepo
kwa mauaji hayo amelitupia lawama jeshi la polisi ambapo amedai kuwa
mbali na matukio ya bodaboda kujeruhiwa,kuuawa na hata kuporwa
pikipiki,kutikisa mji wa Geita wanapowakamata watuhumiwa hao baadaye
huachiwa na kuwatambia mitaani.
Alisema jeshi la polisi ndilo linachangia kuendelea kwa matukio hayo kwa kuzembea kuwachukulia hatua watuhumiwa.
Alisema jeshi la polisi ndilo linachangia kuendelea kwa matukio hayo kwa kuzembea kuwachukulia hatua watuhumiwa.
"Siyo
leo tu ,haya matukio ni ya kila siku lakini cha ajabu tunapowakamata
watuhumiwa,hususani wanaoiba pikipiki zikiwa zimepakiwa na wengine
kujifanya madeiwaka, tunapowafikisha polisi wanaachiwa baada ya siku
mbili,hii inakatisha tamaa sana’’aling’aka Dotto mbele ya mkuu wa
upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Geita.
Kwa
upande wake mkuu huyo wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya
Geita,John Maro akizungumza na bodaboda hao katika mkutano wa dharula
kujadili suala hilo ameahidi kuwapatia ushirikiano na kutishia
kuwawajibisha askari wote watakaobainika kuwakingia kifua waharifu wa
utekaji wa waendesha bodaboda.
Chapisha Maoni