HOME
Umeisikia hii ya waliotaka kuiba sanamu la Bikira Maria kanisani?
Vijana
watatu Songea wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka
kuiba sanamu la Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha
Samora.
Katekista wa Kigango hicho Keneth Mhagama
walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya
ibada ya mkesha ambapo walinzi walifanikiwa kuwadhibiti kabla
hawajafanikiwa na wakawekwa mbaroni.
Vijana hao ni Ahmed, Mohammed na Leonard ambapo Padri wa Kanisa hilo Cristom Kapinga amesema vijana hao wanatakiwa kutubu la sivyo watawaacha kwenye mikono ya sheria washughulikiwe.
Chanzo cha Habari: Gazeti Mtanzania, December 26.
Chapisha Maoni