HOME
KITUO CHA POLISI CHAVUNJWA KWA NGUVU HUKO GEITA
KITUO CHA POLISI CHAVUNJWA KWA NGUVU HUKO GEITA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,jengo lililokuwa
likitumika kama kituo kidogo cha polisi Nkome Tarafa ya Bugando Wilaya ya Geita
limebomolewa na mmiliki wake ili polisi wa kituo watafute sehemu nyingine baada
ya kutokea mvutano katika ulipaji wa kodi ya pango hilo.
Kufuatia
hali hiyo,kwa sasa Mkuu wa
kituo hicho Gwaga Mtawa pamoja na askari wake,hawana mahala pa kuishi
wala
sehemu ya kufanyia shughuli zao za kiofisi,baada ya kutimuliwa na
mmiliki wa Nyumba hiyo kwa kubomoa jengo hilo walilokuwa wamelipanga kwa
miaka mingi sasa
kutokana na kushindwa kulipa kodi kwa kipindi cha miaka mitatu.
Hali hiyo inatokana na Mmiliki
huyo,Siki Deusi Mkazi wa Katoro kubomoa sehemu ya nyumba hiyo,baada ya
kuonekana mwelekeo wa polisi kumlipa kushindikana.
Akizungumza na Malunde1 blog,Deusi alisema anadai kodi ya sh.3.3 Milioni za miaka mitatu na kwamba
amechukua hatua hiyo baada ya kuona askari wanatumia ubabe hasa wakati
anapoenda kudai fedha hizo.
‘’Nimehangaika mno kudai kodi yangu…sijalipwa
kila nikidai ni propaganda tu..kuna siku nilienda kudai wakasema wanakaa kikao
na wafanyabiashara,lakini hawakunilipa.Na hata nilipowaomba wanilipe hata mwaka
mmoja waendelee kukaa hakuna’’
‘Sasa nikiwadai
wananitishia,wanasema na mimi ni miongoni mwa wafanyabiashara tunaolindwa na
hao askari…nilipoendelea kuwadai wakasema niende mahakamani..kwa hiyo mimi
sikutaka yote hayo hawezi kuishi kwenye nyumba yangu kibabe nimeamua kuivunja
ili waondoke wakatafute sehemu nyingine’’alisema.
Alisema baada ya kuona anadanganywa
kuhusu kulipwa ndipo Januari 20,mwaka huu aliamua kwenda kuvunja,uzio wa nyumba
hiyo,bango la kutambulisha kituo cha polisi,choo na bafu na kuwapa notisi ya
siku tatu wahame kwenye nyumba yake.
‘’Nilifanya kazi hiyo kwa hasira
sana na sikutaka anisogelee mtu..nimeamua kuvunja ili atayeingia nitamjengea
upya na kama watashindwa kutoka kwa siku hizo tatu naenda kung’oa bati,waondoke
kabisa nimechoka kuvumilia’’alisema Deusi.
Alisema alichukua amzi huo baada ya
kuona viongozi wa kijiji na kata hawana msaada kwake kutokana na aliyekuwa
mtendaji wa kata hiyo kuhamishwa na mwenyekiti kumaliza muda wake ambao
walisaini mkataba wa jengo hilo..
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji
hicho,Anjelo Daniel alisema fedha hizo zilikuwepo lakini zilitafunwa na
viongozi wa kata hiyo akiwemo diwani wa kata,kitendo ambacho alidai ni
kuwadhalilisha askari kwa kufukuzwa kutokana na kushindwa kulipa kodi.
Kwa upande wake,Diwani wa kata ya
Nkome,Karema Chilatu ambaye ni miongoni wa viongozi waliokuwepo wakati wa
kusaini mkataba huo alikiri jengo hilo kubolewa kutoka na kushindwa kulipa kodi
kwa mmiliki huyo baada ya mapato ya kulipa kutopatikana.
‘’Askari wetu hao ambao wako
watatu..tuliwaweka pale tangu mwaka 2008,kusubiri ujenzi wa kituo cha polisi
ambacho kipo katika hatua ya kukamilika..Lakini Mmiliki wa nyumba hiyo
alikubaliana na wafanyabiashara kwamba watamlipa..lakini imekuwa kimya na
juzi..juzi alikuja kubomoa’’alisema na kuongeza.
‘’Askari wetu tumeamua kuwatafutia
nyumba nyingine..wakute wanaishi pale,ujenzi wa kituo cha Polisi ukikamilika
watahamia katika jengo lao..kwani walipokuwa pamevunjwa uzio,choo na vitu
vingine na sisi hatuna namna ya kumlipa kwani mapato hakuna’’.
Kamanda wa polisi mkoani
Geita,Joseph Konyo akizungumzia tukio hilo,alikiri jengo hilo kubomolewa na
baada ya serikali ya kijiji kushindwa kulipa kodi kwa kipindi chote hicho.
‘’Suala hili linatokana na serikali
ya kijiji kushindwa kulipa,kwani serikali hiyo ndiyo ilikuwa inawajibika
kufanya hivyo..lakini tayari tumepata nyumba nyingine ambayo askari sasa
wanaishi pale wakati ujenzi wa kituo ukiendelea’’.
Na Victor Bariety-Malunde1 blog
Geita
Chapisha Maoni