HOME
Hujasoma Magazeti leo Jan 10? Nimekuchambulia story kubwa tano kutoka Magazetini, zisome hapa
Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) wanakusudia kupeleka hoja binafsi Bungeni ili kumng’oa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Hawa Ghasia kwa kusababisha vurugu katika uchaguzi na siku ya kuapishwa wenyeviti Serikali za Mitaa.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha CUF, Magdalena Sakaya alisema wameamua hayo baada ya Ghasia mwenyewe kukataa kung’atuka na Rais Kikwete kushindwa kumuwajibisha kwa kushindwa kusimamia uchaguzi.
Sakaya
amesema kuna baadhi ya maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika lakini CCM
ilitangazwa kushinda, huku maeneo mengine ambako vilishinda vyama vya
upinzani lakini wakaitwa Wenyeviti waliokuwa wakigombea kupitia CCM kwa
ajili ya kuapishwa hali iliyopelekea vurugu.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Dar wametangaza kumsaka mtu mmoja raia wa Marekani ambaye anatuhumiwa kumuua rafiki yake, Nadine Aburadas ambaye waliyefahamiana miaka mitatu iliyopita kupitia mtandao wa Facebook.
Mtu huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo
katika hoteli Uingereza na kukimbilia Tanzania ambapo vyombo vya habari
vya Uingereza viliripoti kuhusu mauaji hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa makosa ya jinai, Diwani Athumani amesema kuwa upelelezi kuhusu mtuhumiwa huyo bado unaendelea wakishirikiana na Interpol japo hana uhakika kama mtuhumiwa huyo bado nchini.
Taarifa zinasema mtuhumiwa huyo aliingia
hotelini hapo na marehemu siku ya Desemba 30, siku ya January 1
alionekana akitoka peke yake hotelini hapo, akapanda ndege kwenda
Bahrain na baadaye kuja Tanzania.
HABARI LEO
Mfanyabiashara Seleman Manoti
amepandishwa Mahakama ya Wilaya Ilala kujibu mashtaka ya kujifanya
Ofisa wa Usalama wa Taifa kwa lengo la kudanganya kufanya utapeli maeneo
ya Kariakoo, Dar.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na
kurudishwa rumande kutokana na kushindwa kwa masharti ya dhamana
yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kulipa sh. mil. 1.
HABARI LEO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka
amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo wanamshikilia mwanamke mmoja
anayetuhumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja na mama wa mtoto
huyo kulazwa baada ya kunywa pombe ya ‘mturuku’ nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda huyo amesema mwanamke huyo mtuhumiwa, Anastazia Kadama
aliandaa pombe hiyo ya kienyeji na kuwaalika majirani kumsaidia kulima
shamba lake, lakini ikashindikana kwenda kulima kutokana na mvua kubwa
kunyesha.
Kutokana na kuhofu pombe hiyo kuharibika aliamua kuigawa kwa watu ili wainywe bure ikiwemo mama ambaye mtoto wake alifariki, Magdalena Muna.
Magdalena aliionja pombe hiyo na
kumuonjesha mtoto wake, alianza kutapika na kuharisha, wakiwa njiani
kuelekea Hospitali mtoto huyo alifariki.
JAMBO LEO
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Majengo Moshi, Peter Lyimo
amelalamikia kuwepo utitiri wa vitabu vingi kwamba vinachangia
wanafunzi kufeli katika mitihani yao na kuiomba Serikali kuhakikisha
inaweka mitaala inayoendana na maisha ya Watanzania.
Mkuu huyo wa shule amesema kuwa utitiri
huo wa vitabu unawachanganya wanafunzi ambao wanashindwa kuchagua vitabu
vipi muhimu wasome na vipi wasivisome, huku kukiwa na msululu mkubwa wa
vitabu kuingia sokoni bila kuhakikiwa hivyo wanafunzi kusoma vitabu
vyenye makosa.
Mwalimu huyo amesema kumekuwa siasa
imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kuvuruga mfumo wa elimu ikiwemo
mitaala kubadilishwa mara kwa mara hivyo kuwachanganya walimu na
wanafunzi.
Chapisha Maoni