HOME
TANZANIA DAIMA
Siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza nia ya kuwania Urais, Sheikh Shariff Matongo ameibuka na kusema mmoja wa viongozi anayewania nafasi hiyo ya juu atafariki dunia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yahesabu za Serikali Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya trilioni 1 katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
“Najua bado mnalia kuhusu bombala kupeleka gesi Dar es salaam,machozi yenu yatafutika kwani tayari habari ya ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hilo zimeanza kuchomoza.”– Zitto.
“Kiongozi wa Upinzani Mbowe ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi kuhusu ujenzi wa bomba hilo,na pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia,tunaamini gharama za mradi huu zimezishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya dola milioni 600 sawa na zaidi ya trilion 1“alisema Zitto.
Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 1, 2015
TANZANIA DAIMA
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila
amesema kuwa mwaka 2015 ni mgumu kwani Serikali ipo taabani kifedha
kiasi cha kusitisha kandarasi ya barabara kutokana na ukata.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania
wanakusanya bilioni 800 kwa mwezi wakati mahitaji ya mishahara pekee ni
takribani bilioni 500 na kwamba kiasi cha bilioni 300 kinachosalia
hakitoshi hata kununua karatasi na mafuta ya kuendesha ofisi za Serikali
nchi nzima.
Alisema Serikali iko katika hali mbaya
wakati iko kwenye kutaka kutekeleza mambo makubwa yanayohitaji fedha uku
mwaka huu ukiwa ni wa uchaguzi ambao ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.
MTANZANIA
Hali si shwari ndani ya chama cha
Alliance for Change ACT baada ya kuwafukuza uanachama aliyekua Katibu
mkuu wake Samson Mwigambana mshauri wa chama hicho Profesa Kitila
Mkumbo.
Mbali na hao viongozi wengine
waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja na aliyekua Makamu Mwenyekiti bara
Shabaan Mambo,Mwenyekiti wa Wazee Wilson Muchumbusi na katibu wa vijana
Philip Malaki.
Mwenyekiti wa ACT Kadawi Lukas alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuitishwa kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana.
“Tumewavua
uongozo na kuwafukuza uanachama Kitila na Mwigamba kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo ya kutumia madaraka vibaya kwa kukabidhi chama kwa
mafisadi.“
Alisema viongozi hao walisaini
makubaliano ya kuendesha shughuli za chama ikiwemo kusimamia mikutano
na uchaguzi bila kushirikisha viongozi wengine.
NIPASHE
Ulazaji wa bomba la maji la Mamlaka ya
majisafi na majitaka Dar es salaam Dawasa katika mradi wa Ruvu chini
kuanzia Bagamoyo hadi Dar umekamilika kwa asilimia 93.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika March
na utakua ukitoa maji lita milioni 270 kwa siku katika maeneo mbalimbali
ya Jiji na sehemu ambazo bomba linapita.
Dawasa imesema kuwa mradi huo umefikia
hatua hiyo baada ya jitihada za kutatua mgogoro huo kwa kuzungumza na
wakazi ambao bomba hilo linapita ambao walifungua kesi mahakamani
kuupinga wakidai walipwe fidia.
Menejamradi huo Romanus Mwangingo alisema kuwa mradi huo unatazamiwa kukamilika baada ya kulaza bomba katika maeneo yote.
NIPASHE
Mbunge waviti maalum kupitia UVCCM Mkoa
wa Arusha Catherine Magige amelalamikiwa kwa kuwagombanisha viongozi wa
Jumuiya ya wanawake UWT Mkoa wa Arusha kutokana na kinachodaiwa kuwa ni
mbio zake za ubunge kupitia Jumuiya hiyo.
Mgongano huo unadaiwa kutokana na
ukiukwaji wa kanuni kilichofanywa na Mbunge huyo kwa kugawa zawadiza
vitenge na mchele kwa ajili ya sikukuu za Krismass kwa viongozi wa
Jumuiya hiyo bila kuutaarifu uongozi wa juu.
Pia kamati hiyo imemfungia ofisi Katibu
wake Stamil Dendegu kwa tuhuma za kumruhusu Magige kugawa zawadi na
kumkaimisha ofisi katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Fatma Hassan.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Flora
Zelote alikanusha kusimamishwa kazi kwa katibu wake wala kuwepo kwa
kikao kilichomjadili yeye.
NIPASHESiku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza nia ya kuwania Urais, Sheikh Shariff Matongo ameibuka na kusema mmoja wa viongozi anayewania nafasi hiyo ya juu atafariki dunia.
Sheikh Shariff alitoa utabiri huo juu
ya ndoto zilizomjia usiku na kuoteshwa mambo zaidi ya matano
yatakayoikabili nchi mwaka huu.
Alisema atakayefariki dunia ni yule
mgombea anayewania nafasi ya urais ambaye alishawahi kuwa kiongozi
katika nyadhifa mbalimbali kupitia CCM.
“Ndoto
yangu nilioteshwa sikukaa nayo peke yangu niliwaeleza Masheikh
mbalimbali kutoka Abu Dhabi, Nigeria na kupata ushauri wao na
wakaniambia suala hilo nisikae nalo bali niwashirikishe Watanzania wenzangu“alisema.
MWANANCHIMwenyekiti wa Kamati ya Bunge yahesabu za Serikali Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya trilioni 1 katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
“Najua bado mnalia kuhusu bombala kupeleka gesi Dar es salaam,machozi yenu yatafutika kwani tayari habari ya ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hilo zimeanza kuchomoza.”– Zitto.
“Kiongozi wa Upinzani Mbowe ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi kuhusu ujenzi wa bomba hilo,na pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia,tunaamini gharama za mradi huu zimezishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya dola milioni 600 sawa na zaidi ya trilion 1“alisema Zitto.
Alisema katika miakaya hivi karibuni
Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa na gesi na
wananchi wameonekana kuwa wanaweza kupigania maslahi ya Taila lao.
MWANANCHI
Timu ya Makachero wa Polisi kutoka Dar
es salaam imewasili Mwanza kuongeza nguvu za kumsaka mtoto mlemavu wa
ngozi Pendo Emmanuel anyesadikiwa kutekwa akiwa nyumbani kwao.
Polisi wametangaza dau la milioni 3 kwa atakayewezesha kutoa taarifa za waliohusika kufanya tukio hilo la kumteka mtoto huyo.
Hata hivyo taarifa zilipatikana jana
zinasema tayari watu sita wameshikiliwa na polisi wakishusishwa na tukio
hilo akiwemo baba wa mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Valentino Mlowola ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia Makachero
wa Mkoani Mwanza kuhakikisha mtoto huyo anapatikana aidha akiwa amekufa
ama akiwa hai.
Chapisha Maoni