HOME
Panya road watingisha Dar, Wafanya uporaji, Wananchi wakimbia ovyo
Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena, taharuki,
hofu na wasiwasi mkubwa viliwakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa
saa mbili baada ya kundi maarufu la waporaji la Panya Road, kuvamia
mitaa mbalimbali na kupora mali.
Taarifa za kundi hilo lililopora watu katika
baadhi ya maeneo ya jiji hilo zilienea kwa kasi ya ajabu kupitia
mitandao ya kijamii watsap, twitter, jamii forum, blog, instagram na
ujumbe mfupi wa simu.
Baada ya maeneo ambako kundi hilo linadiwa kufanya
uporaji ni Tabata, Magomeni Kagera, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni,
Kijitonyama, Manzese, Kigogo na Buguruni, huku wanafunzi wanaoishi
katika Hosteli za Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakitoka nje ya mabweni yao
kwa kuhofia kuvamiwa na kikundi hicho.
Taharuki hiyo iliyoanza saa mbili usiku,
ilisababisha wakazi wa maeneo mengi ya jiji kujifungia ndani, huku
wafanyabiashara wakifunga maduka na kujificha wakihofia kundi hilo la
wahalifu.
Chapisha Maoni